WADAU WA PSPF WAONESHWA NYUMBA ZA MKOPO ZILIZOPO BUYUNI CHANIKA
Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi
wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka
2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii
kwa ujumla.
Mikoa
iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam –
Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora –
Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).
Aidha
kwa Muji wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu
amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la
mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne
ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa
ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.
Gharama
ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya
Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo
la Thamani.
Comments