Kila mtu achinje na kula, mradi asivunje Sheria

Na Bryceson Mathias
Nianze kwa kusema hivi Bundi aliyeiandama Imani ya Madhebu yetu kwa lengo tu la kuboresha maslahi ya mtu aliyeasisi hoja ya kuchinja ili watanzania waingie katika malumbano, sasa afahamu hoja yake ya uchovu imeshindwa.

Haiingii akilini kwa mtu anayetegemewa, mwenye nafasi na dhamana kubwa iliyotukukuka, iwe ki-Imani au Ki-Itikadi, kuibua migogoro ya dini mithili ya David na Mary katika kitabu cha Kingereza tulivyosoma hapo kale kidogo, walivyogombea Mtoto na kumvuta mikono hadi ikakatika.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikiliza na kusoma malumbano ya kuchinja nikabaini katika suala la hilo mmoja wetu miongoni mwa pande zinazobishishania uhalali huo; anavutia kamba upande wakebadala ya kukaa meza moja na kutengeneza maridhiano.

Kilichopelekea mgogoro huu hasa, yawezekana kabisa umetokana na kupotoka kwa baadhi ya dni ambazo pengine zinajiona ni bora kuliko Dini nyingine, huku wakisahau kujali kwamba wenzao wenye miiko ya dini zao ya kutokula kitoweo kilichochinjwa au kutochinjwa na dini nyingine.

Kwa mfano; kwa mila na desturi katika Jamii au familia, kuna watu hawali vitu fulani fulani kama Njiwa, Kuku, Bata, Nyama, Samaki na vitu vingine katika koo na familia zao. Hivyo hatupaswi kuwalazimisha au kuwapuuza kwa kile wanachokiamini, na akitokea mtu wa namna hiyo atakuwa Mkorofi.

Kimsingi kwa ukweli halisi, Serikali haitakiwi kubabaika kiasi cha kuuma maneno na kukaa kimya, bali isema wazi kwamba kila mtu anaweza kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu havunji sheria za nchi kwa maadili yoyote.

Je; mtu akila Mlenda nyumbani kwake au akaamua kuchinja Kuku, Bata, Njiwa, Mbuzi au kitoweo chochote alichonato, kuna ulazima wa kumlazimisha achinjiwe? Je tuna haja ya kumlalamikia na kumtuhumu kiasi cha kumsababishia ghasia na magombano akiwa ametulia kwake?
Mu- Islam akichinja na kula nyumbani kwake bila kuathiri wakristo; Wakristo wana sababu ya kumlalamikia na kumtuhumu kwa vurugu? Vivyo hivyo Mkristo akichinja mnyama wake kwake bila kuathiri Wa-Islam; Wa-Islamu wana haja ya kuwafanyia vurugu na vitimbwi wakristo? La hasha!


Lakini nakubaliana kwamba, Mfanya Biashara wa Kikristo au Wa K-Islamu, akitaka kufanya Biashara ya Nyama, Sherehe, Msiba, au kusanyiko lolote linalohusisha Kula, ni lazima uchinjaji wa kitoweo chake uhusisishe ridhaa ya uchinjaji ambao utaruhusu Watu wote kwenye kusanyiko hilo kula.

Kwa maana hiyo viongozi, wananchi na waumini wa madhehebu mbalimbali nchini waelewe kwamba, Wapagani, Wakristo, Wa-Islamu wanaweza kuchinja kitoweo chao na wakala endapo wako katika familia zao, kama ilivyokuwa ikifanyika hapo awali bila kuathiri chochote ili mradi havunji sheria za nchi.

Hivi kama huli kitu, na wengne wanakula, kwa nini upate uchoyo na uroho wa kutaka kula kwa tamaa yako? Mimi sioni kitu hapa maana hakuna Mkristo au M-Islam ambaye ni bora kuliko mtu wa Dini zingine, hiyo inatokana na miiko au mila za dini zao za kutokula vitoweo vilivyochinjwa na dini nyingine.

Mbona huko Ulaya, wenzetu wana maduka ya Bucha ambapo Wakristo wana ya kwao wananunua wanachokita na wa- Islamu wana ya kwao wanunua wanachokita kwa nini sisi tugombane hata kwa vitu ambavyo hatuvili? ningekuwa mimi, akichinja Mu-Isalmu nakula; maana najua jinsi ya kufanya ili nile

Hivyo Usichokula usikionee uroho na tamaa ya kukila, na pia tusiwabeze wanaokula.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA