TIMU NNE MPYA KUINGIA KIPINDI CHA MWISHO CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ AFRIKA MASHARIKI
Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tano cha
Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka
Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania – bluu, Uganda- kijani na nyeusi.
April
10, 2013, Dar es Salaam; Jumatano
iliyopita katika sehemu ya nne kupitia televisheni za ITV na Clouds TV,
mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus
Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya
tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa, baada ya kuwapiga chini
timu za Tanzania na Uganda. Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi
kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama
nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya
walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta
wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani 1,500.
Enphatus na Samwel wana
nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo
wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita
cha fedha za kimarekani hadi kufikia
dola 250,000. Washiriki bora watakwenda kukutana uso kwa uso na mashabiki
wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Tanzania, Kenya, na Uganda ili atakayeonesha ufahamu na ujuzi zaidi wa
soka atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa
ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi
kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15)
usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku
.
Katika
kipindi cha tano cha mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni
vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu
ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu
yote yatapatikana Jumatano hii.
Timu ya blu-Tanzania:
·
Khenry Sadallah(26) na
Abubakari Mohamed(19) kutoka
Dar-es-Salaam watashiriki katika sehemu ijayo. Harry atakuwa kichwa cha timu
ambaye ni mshabiki wa AC Milan wakati Abubakari
ambaye ni mwanafunzi na mshabiki wa Manchester United ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira
Timu nyekundu-Kenya:
·
Ken Muturi (26) na Chris
Mwamgi (19) wote kutoka Nairobi wanamatumaini makubwa yakuwa timu ya mwisho
kuingia kwenye mashindano ya Pan African. Ken ni mfanyabiashara kwa njia ya mtandao, ni mpenzi
wa mpira wa miguu ambapo atakuwa kichwa cha timu wakati Chris ambaye ni
mchezaji wa Springland FC ataonesha kipaji chake cha mpira wa miguu.
Timu ya kijani-Uganda
·
Mfanyabiashara Ian Ford(24)
na mwanafunzi wa uchumi Herbet Odipio(23) kutoka Kampala ni mashabiki wa
Manchester United watashiriki katika kipindi kijacho cha mashindano Guinness
Football Challenge. Ian atakuwa kichwa cha timu wakati Herbet ataonesha uwezo
wake wa kusakata kabumbu.
Timu
nyeusi-Uganda:
Edward
Lyukamuzi(23) na Timothy Nimungu(22) kutoka Kampala ni timu ya pili kutoka
Uganda watashiriki kipindi cha 5 cha mashindano haya. Edward ni mtaalamu wa
Teknolojia ya mawasiliano ndiye kichwa cha timu wakati Timothy ambaye ni
mtaalamu wa masoko atonesha uwezo wake wa kucheza soka.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa
kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa njia ya mtandao. Wanaweza kufanya
hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika
tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya,
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari
zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia
na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya
bia uipendayo ya Guiness wakati
unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa
walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.
Tafadhali Kunywa kistarabu.
Note:
Comments