UINGIAJI MAGARI WAONGEZEKA BANDARINI DAR

                                                                    Bandari ya EDar es Salaam

Dar es Salaam. 
Kumekuwa na ongezeko kubwa la takriban asilimia 50 la magari yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kinachoelezwa kuwa matokeo ya uboreshaji wa huduma na usalama katika bandarini hiyo.

Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), zinaonyesha kuwa magari yanayopita Bandari ya Dar es Salaam, yameongezeka hadi kufikia 83,440 kwa kipindi cha miezi minane kilichoishia Februari mwaka huu.

Magari hayo yameongezeka kutoka magari 55,819 kwa kipindi kama hicho kilichoishia Feburuari 2012.

Takwimu hizo za TPA zinaonyesha kuwa kwa kipindi cha kati ya Julai mwaka 2012 na Feburuari mwaka 2013, Bandari ya Dar es Salaam ilihudumia magari 83,440 yaliokuwa yanaingia nchini na yale yaliyokuwa yanapelekwa nchi jiran.

Februari mwaka huu takriban magari 10,000 yalipokelewa.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi, alisema ongezeko magari, limechangiwa na uwekezaji mkubwa katika vitendea kazi na mafunzo kwa wafanyakazi.

Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni ilitangaza ongezeko kubwa la mizigo inayohudumiwa na kueleza kuwa ongezeko hilo la biashara ni matokeo ya ufanisi wa kazi uliotokana na uwekezaji.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari imewekeza kiasi cha Euro milioni 10.4 (zaidi ya bilioni 20 za Kitanzania) katika ununuzi wa mitambo ya kisasa ya kupakia na kupakua mizigo katika bandari zake za Dar es Salaam na Tanga. TPA pia imewekeza katika mafunzo kwa wafanyakazi, hatua ambayo imeripotiwa kuongeza morali ya kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI