Mapenzi
ni dhana pana sana. Ni dhana ambayo mpaka hivi leo mwanadamu bado
anahangaika kupata ufafanuzi wake. Hata hivi leo tukiuliza hapa hivi
mapenzi ni nini,tunaweza kupata maoni zaidi ya hata elfu moja huku kila
mmoja akiwa na maana au tafsiri yake kuhusu mapenzi. Usishangae kama
tafsiri hiyo yaweza kuwa tofauti kabisa na yako au yangu!
Bahati
nzuri au mbaya ni kwamba mwisho wa siku wote tutakuwa sahihi. Kila
mmoja anaruhusiwa kutafsiri dhana ya mapenzi au penzi kwa kadri
anavyoona yeye au kwa jinsi ambavyo “mvua inakuwa imemnyeshea”.Si
unakumbuka kwamba aisifiaye mvua imemnyeshea?
Upana
wa dhana ya mapenzi huenda ndio hupelekea kila kukicha wanamuziki
wanazidi kutunga na kuimba nyimbo kuhusu mapenzi. Mapenzi hayajaanza
jana wala leo na hayatokaa yafikie mwisho.
Pamoja
na hayo, zipo nyimbo za mapenzi ambazo wenzetu wanaotumia kizungu huwa
wanasema “it has stood the test of time” kumaanisha kwamba wakati sio
kitu kwake kwani kitu hicho(nyimbo) bado kinapendwa na kitaendelea
kupendwa kwa wakati mwingi ujao.Mfano mzuri wa nyimbo za aina hiyo ni
ule uitwao Maria (Mary Maria) ulioimbwa na Vijana Jazz Band enzi hizo ikiwa chini ya uongozi wa Hayati Hemed Maneti(pichani).
Katika wimbo huo utamsikia Maneti akilalama kutokana na penzi zito
alilonalo kwa “mtoto” Mary. Baadhi ya maneno kwenye wimbo huo ni kama;
Kwa kweli sasa nimenaswa
Sina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh
Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeeeSina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh
Na wala sitapenda mpaka nife,
Mpaka nife, mama Mary oooh
Bonyeza
player hapo chini upate burudani kamili ya wimbo Maria.Kama unaye
umpendaye, huku naye anakupenda kwa dhati na wala sio “for convenience”
basi muite mwambie mcheze kidogo wimbo huu.Nakutakia Ijumaa Njema.
Comments