MBUNGE WA UKONGA ATEMBELEA MIRADI YA MFUKO WA JIMBO.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la Ukonga ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo Eugene Mwaiposa (wapili kulia) akimsikiliza kwa makini Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mzambarauni ya Ukonga Magnus Kayombo, jijini Dar es Salaam, wakati akimweleza maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya walimu wa shule hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya ujenzi wa ofisi hiyo. Gharama za ujenzi huo zinakadiriwa kufikia Tsh.60Millioni..

Mkuu wa Shule ya Mzambarauni Magnusi Kayombo akiwaongoza wanakamati ya mfuko wa maendeleo ya Jimbo la Ukonga kukagua mandeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo.
Wakisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu huyo wa Shule.
Baadhi ya wanakamati ya shule nao walikuwepo kuilezea kamati ya maendeleo ya mfuko wa jimbo hilo juu ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo mbunge huyo amewaomba wahisani zaidi kujitokeza kusaidia maendeleo ya ujenzi huo.
Eneo ambalo linahitajika daraja lakini kutokana na uchache wa fedha wamelazimika kujenga kivuko kidogo cha kawaida kwaajili ya wananchi wa eneo la Kivule kwenye eneo la Mto Mzinga kwenye jimbo hilo, Wananchi wa eneo hilo wamekua wakipata tabu wakati wa mvua kutokana na kutokuwepo kwa kivuko.
Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akikagua mradi wa ujenzi wa kivuko eneo la Kivule wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali jimboni humo.
Ujenzi wa kivuko hicho ulisimama kutokana na mvua zilizozikiendelea kunyesha na kazi ya umaliziaji inatarajiwa kuendelea hivi karibuni.
Ujenzi wa kituo hiki kikuu cha Polisi eneo la kata ya Chanika nao unaendelea kwenye awamu ya pili ya ujenzi ambapo kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo hilo ilifika kukagua.
Maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo yalitolewa mbele ya kamati.
Kwenye ziara hiyo alikutana na wanachama wa chama cha Mapinduzi ambao walisimamisha ziara yake ili awasalimie na baadaye  kuendelea na ziara hiyo.
Iyena Iyena zikapambamoto!

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA