MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI

Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Jamhuri  hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
 Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB  kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
 Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE