KAMPUNI YA GREEN WASTE YAKABIDHI NDOO 16 SHULE YA BUNGE NA KUFANYA USAFI

IMG_9383  
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph (katikati) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wanafunzi na walimu wakifanya usafi katika mazingira ya shule ya msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katika kati ya jiji la Dar es Salaam.
IMG_9402
Mkusanyaji wa Mapato wa kampuni hiyo Bw. Almachlus Rwakatale akikabidhi jumla ya ndoo 16 za rangi kwa Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya. Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph.
IMG_9368
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph na Mkusanyaji wa Mapato wa kampuni hiyo Bw. Almachlus Rwakatale wakishirikiana na uongozi wa shule ya msingi Bunge katika zoezi la upandaji miti kwenye maeneo mbalimbali yanayoizunguka shule hiyo.
IMG_9376
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph na Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya wakishirikiana kumwagilia maji moja ya miti waliyopanda katika shule hiyo kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
IMG_9380
Zoezi la usafi likiendelea kwa kushirikiana na Walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
IMG_9390
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katikati ya jiji la Dar es Salaam na safari hii wametoa ndoo 16 za rangi katika Shule msingi Bunge.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO