MJENGWA BLOG YATIMIZA MIAKA 7, MKURUGENZI APONGEZ WADAU



Mmiliki  wa  mtandao  wa Blogu  ya Mjenga  amepongeza  jitihada  kubwa ambazo zimefikiwa katika blogu  hiyo ikiwa ni pamoja  na kuwapongeza  wadau mbali mbali ambao  wameendelea  kutembelea  blogu  hiyo maarufu nchini Tanzania.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni  hiyo Maggid Mjengwa(pichani) ameyasema  hayo leo katika hafla  fupi  ya kuadhimisha miaka 7 ya  mtandao huo pendwa hapa  nchini.

Mjengwa amesema  kuwa katika nchi mbali mbali ambazo amepata  kupita jina la Mjengwa  Blogu   na jina la FrancisGodwinBlog kwa mikoa ya nyanda za juu kusini  yamekuwa  yakitajwa na watanzania mbali mbali.


Ndugu zangu,
Kwa mwanadamu, hakupaswi kuwapo na ukomo wa kujitahidi kufanya yalo mema kwa jamii yako.
Na katika kujitahidi kuyafanya yalo mema, basi, mwanadamu uwe tayari kukumbana na changamoto nyingi. Na kama  ilivyo kwa maji ya mto, yanapokutana na mwamba, basi, kasi yake huongezeka maradufu.
Leo blogu yako hii ya Mjengwablog imetimiza miaka saba. Miaka saba si haba. Ni umri wa mtoto kuanza shule.
Kwa niaba ya timu nzima ya Mjengwablog nachukua fursa hii kuwashukuru kwa dhati ’ WanaFamilia’ wote wa Mjengwablog kwa kuwa nasi katika hali zote. Hivyo basi, kutuunga mkono.
Naam, ni miaka saba ya kuwa mtandaoni karibu katika kila siku inayotujia na kupita. Ni miaka saba ya mapambano magumu ya kuitumikia jamii na kuhakikisha kuwa tunabaki hai.
Maana, unapoamua kuitumikia jamii bila kuegemea upande, basi,  ina maana pia ya kujiweka  katika mazingira ya hatari sana.  Yumkini kuna maua mengi ya upendo yanaweza kurushwa kwako, lakini, kuna mishale michache ya sumu ambayo pia itarushwa kwako. Kwamba kuna maadui pia.
Na ukimwona nyani ametimiza miaka saba , basi, ujue kuna mishale  kadhaa ameikwepa. Lakini, na anavyozidi kuendelea kuishi, yumkini kuna mishale mingine inaandaliwa. Na nyani hatakiwi kuishi kwa kuogopa mishale ya wanadamu. Vinginevyo, ajitundike mtini, afe.
Lililo jema na kutia faraja ni kutambua, kuwa kuna walio wengi wenye kufaidika na kazi hii ya kijamii ambayo Mjengwablog inaifanya.  Ni hawa ndio wenye kututia nguvu ya kuendelea kuifanya kazi hii pamoja na changamoto zake nyingi.
Ndugu zangu,
 
Ilikuwa ni Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi wa blogu. Ni picha hiyo inayoonekana hapo juu. Niliipiga eneo la Kinondoni Shamba. 
Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya wale ambao sauti zao hazisikiki.
Na Mjengwablog ikawa chachu ya kuanzishwa kwa gazeti la michezo na burudani la ’ Gozi Spoti’, ikawa chachu pia ya kuanzishwa gazeti la ’ Kwanza Jamii’.
Na kuna miongoni mwetu wenye kufikiri, kuwa mwenye kumiliki gazeti ni lazima awe Mhindi au Mtanzania ’ mweusi’
 Mfanyabiashara tajiri. Nakumbuka kuna hata ambao hawakuwa tayari kuchangia kiuandishi kwenye ’ Gozi Spoti’ na ’ Kwanza Jamii’ kwa vile linamilikiwa na ’ Mswahili mwenzao!’Na hata kupata matangazo kukawa na ugumu mkubwa. 
Gozi Spoti lilisimama kuchapwa baada ya mwaka mmoja mitaani.
 Kwanza Jamii, nalo likasimama kuchapwa. Likarudi tena baada ya kuingia  ubia na Shirika la Daraja. Baada ya miaka miwili na baada ya aliyepelekea kuingia ubia  kuondoka nchini na kurudi kwao Uingereza, basi, Kwanza Jamii nalo ’ likaandaliwa’ mazingira ya kuondoka mitaani.
 
 Hata hivyo, Kwanza Jamii, gazeti dogo, ambalo  naamini ni muhimu kwa jamii, limerudi tena kupitia mtandaoni. Mipango iko mbioni kuliimarisha zaidi katika siku zijazo.
Ndugu zangu,
 
Changamoto zipo ili tukabiliane nazo, na si kukata tamaa. Mjengwablog inatimiza miaka saba leo kwa vile  tulishaamua, kuwa  tutapambana hadi risasi ya mwisho. Hivyo pia, tutapambana hadi pumzi ya mwisho.
Maana, tunaamini kuwa kazi tuifanyayo ni yenye manufaa kwa jamii pana. Na tuna haki ya kuifanya. Tunavumilia sauti zenye kutushutumu na kutukosoa. Kuna tunayojifunza kutoka kwa wakosoaji wetu. Tunawashukuru sana na tunawaomba waendelee kutukosoa kila wanapoziona kasoro.
 Lakini, kuna wachache pia wenye kuonyesha zaidi chuki kuliko kukosoa.  Hawaipendi kazi tuifanyao wala kuithamini, ni kawaida. Lakini, faraja ni kutambua kuna wenye kuipenda na kuithamini kazi yetu.
 Hapa chini ni mmoja wa watu hao;
Maggid,
Iringa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA