MATOKEO YA UTAFITI WA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA 800 ULIOFADHILIWA NA TBL YAKABIDHIWA KWA KAMANDA WA KIKOSI CHA POLISI CHA USALAMA BARABARFANI,DCP, MPINGA

 Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akimkabidhi Kamanada wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, taarifa ya zoezi la upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na malori iliyofanywa wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha Mizani cha Mikese, mkoani Morogoro mwaka jana. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo. TBL ilifadhili zoezi hilo.
 Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila (kushoto) akimkabidhi Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, taarifa ya zoezi la upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na malori lililofanywa wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha Mizani cha Msata, mkoani Pwani mwaka jana. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo.

 Afande Mpinga (wa pili kulia) akiwa na Kilindo wa TBL pamoja na madakari  waliowasilisha utafiti huo. Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi  na Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kulia) akizungumza baada ya madaktari wa Hospitali za Tumbi na Morogoro (hawapo pichani), kukabidhi matokeo ya upimaji wa afya za madereva 800 mabasi ya abiria na malori wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani, mwaka jana katika vituo vya mizani vya Mikese Morogoro na Msata Pwani. Zoezi hilo lilifadhiliwa na TBL. Aliyepokea taarifa ya matokeo hayo, Dar es Salaam juzi,  ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu na Berther Mturi wa TBL.
Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila  (katikati), akielezea jinsi walivyoendesha zoezi hilo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria. Steve Kilindo pamoja na Afande  Kahatano wa kikosi cha usalama barabarani Makao Makuu.
  Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akielezea jinsi walivyofanya utafiti huo.
 Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (katikati) akielezea kufurahishwa na matokeo ya utafiti huo.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia), akionesha moja ya matokeo ya utafiti. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO