Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva:'“Tumeanza mchakato wa kuboresha daftari kwa kuanza kuhakiki vituo vya uandikishaji wa kupiga kura vitakavyoongezeka kwa lengo la kuvisogeza karibu zaidi na wananchi,”

Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva.
---
 Pamoja na kushindwa kutaja tarehe rasmi ya kuanza kuboresha daftari la kudumu la wapigakura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema daftari hilo litaboreshwa kabla ya kuanza kwa upigaji wa kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Upigaji wa kura hiyo utafanyika ndani ya siku 70 baada ya kumalizika kwa Bunge Maalumu la Katiba linalotarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao mjini Dodoma. Litafanyika kwa kati ya siku 70 na 90.

Nec imetoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wananchi kwamba tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, daftari hilo halijawahi kuboreshwa, jambo ambalo litasababisha upigaji wa kura kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kutawaliwa na vurugu. Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu waliotimiza umri wa kupiga kura lakini hawamo katika daftari hilo.Pia waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura na wenye kasoro mbalimbali zinazowafanya wapoteze sifa.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.......

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA