Tanzania yaitaka Miss World 2027! Dkt. Samia Afanya Mazungumzo Ndoto ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya urembo, Miss World 2027, imechanua baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanya mazungumzo muhimu na uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited. Kikao hicho cha kihistoria kilifanyika Julai 20, 2025, huko Kizimkazi, Zanzibar. Uongozi wa Miss World Limited uliongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake, Bi. Julia Evelyn Morley, akiambatana na mshindi wa taji la Miss World 2025, Bi. Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, pamoja na Miss World Africa, Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia. Mazungumzo hayo, ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na viongozi wa Maliasili na Utalii, yalilenga kujadili namna Tanzania inavyoweza kuandaa kwa mafanikio makubwa mashindano hayo makubwa ya kimataifa. Mazungumzo haya kati ya Rais Dkt. Samia na uongozi wa Miss World yana...
Comments