MTOTO WA MGIMWA ASHINDA KURA ZA MAONI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA



 Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi ya baba yake kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Na Francis Godwin, Iringa

Mtokeo  ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo  huku mtoto wa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga  akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  katika  ukumbi wa shule ya  sekondari  Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata  kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA

JESHI LA POLISI LATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA, LAONDOA KIZUIZI CHA KUTOTOKA NJE BAADA YA SAA 12 JIONI