WANANCHI WAMSHITAKI TUNDU LISSU KWA KINANA KWA KUKWAMISHA MAENDELEO YAO KWA MIAKA MINNE

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Katika Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema, Kinana alishuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ujenzi wake umekwamishwa na mbunge huyo kwa kuwzuia wananchi kuchangia fedha za miradi hiyo akidai kuwa fedha zote zitatoka serikalini.



Baadhi ya miradi iliyosimama aliyoikagua Kinana, ni Zahanati ya Kimbwi ukiwemo ujenzi wa nyumba za waganga ambayo imeishia kwa kupigwa msingi wa zege. Vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Unyaghumpi ambapo walikutwa watoto wa shule ya awali wakifundishwa huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu kukiwa wazi bila kuzekwa.


Miradi mingine iliyokwama ni ujenzi wa barabara, mawasiliano ya simu, maji na umeme

 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida, Sija Lukwale akiungana na wananchi kusaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba la Bibi Mjane, Mayasa katika Kijiji cha Unyaghumpi, katika jimbo hilo la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema la Singida Mashariki.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, kutoka Zanzibar, Khadija Aboud Hassan akiungana na wananchi kuvuna uwele na mtama katika shamba la Bibi Mjane, Mayasa.
 Sehemu ya mtama na uwele uliovunwa na Kinana na msafara wake katika shamba la Bibi Mjane Mayasa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA na kutukana matuzi bungeni.
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida Agriculture, Ally Mohamed  jinsi wanavyozalisha maharage kwenye shamba la kumwagilia lenye ukubwa ekeli 200 katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi, Singida.
 Wafanyakazi wa shamba hilo, wakichuma maharage katika shamba hilo.
 Kinana akikagua shamba la maharage katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi. maharage hayo huuzwa nje ya nchi.
 Wafanyakazi wa shamba hilo wakimwagilia dawa kwenye shamba la maharage
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba hilo wakiwa wamebeba ndoo zenye maharage hayo tayari kuyapeleka kwenda kufungasha kwenye makasha tayari kusafishwa kwenda kuuza nje ya nchi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nanuye akitumia treka kulima shamba la kampuni hiyo
 Kinana akisaidia kufungasha maharage hayo, kwa ajili ya maandalizi ya kuuza nje ya nchi.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.
                                              Maharage yakiwa kwenye kasha
                                             Nape akisaidia kuchambua maharage
 Kinana akiangalia makasha yenye maharage yaliyohifadhiwa kwenye kontena lenye jokofu linalotumika kusafirishia nje ya nchi.
 Msindai akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo aliwakataza wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Msingi wa jengo la madaktari ukiwa umeachwa bila kujengwa nyumba, kwa takribani miaka mitatu sasa, tangu Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi ya maendeleo jimboni humo.
 Jengo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari.
 Kinana (kulia) na Nape pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Msambya wakiondoka baada ya kukagua  zahanati hiyo isiyotumika.
 Wananchi wakijitolea kukwatua nje ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi Unyaghumpi ambayo ujenzi wake ulikwamishwa na Tundu Lissu.
 Wananchi wakiwa wamejipanga kusomba matori ya kujengea vyumba vya madarasa vya shule ya Unyaghumpi, wakati wa ziara ya Kinana wailayani Ikungi.

 Wanafunzi wa elimu ya awali, wakifundishwa na mwalimu Juliana Joseph huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu ya paa kukiwa wazi katika moja ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi vilivyozuiliwa kujengwa na Mbunge Tundu Lissu kwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha na kuwaambia kuwa fedha zote zitatoka serikalini.
 Kinana akilakiwa na ngoma ya asili alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu, katika Jimbo la Singida Mashariki la Tundu Lissu wa Chadema.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu wilayani Ikungi.
 Mfuasi wa Chadema akihudhuria mkutano wa CCM uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  Mjini Ikungi, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi, Jimbo la Singida Mashariki na kuwataka wananchi wamhoji kama kuna miradi aliyoitekeleza wakati wa awamu yake hii ya ubunge wa jimbo hilo.
 Nyaraka mbalimabli ikiwemo bendera ya Chedama vikiwa vimetupwa chini na Ismail Gwau aliyekuwa Katibu wa Tawi la Chadema wilayani Ikungi, ambaye aliamua kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara.
 Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akinyoosha juu ya kadi ya CCM  aliyokabidhiwa na Kinana  alipojiunga na CCM katika Mkutano huo wa hadhara.
 Wanachama wapya na wa zamani wa CCM wakila kiapo cha utii katika mkutano huo.
Kinana akiawa na baadhi ya vijana waliomzonga baada ya kumalizika kwa mkutano mjini Ikungi, Jimbo la Singida Mashariki.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

DK NCHIMBI AKAGUA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA CCM MKOA WA GEITA

MAMILIONI YA CCM YATUA AKAUNTI YA TUNDU LISSU

ASKOFU CHANDE AISHUKURU SERIKALI KULIPATIA USAJILI WA KUDUMU KANISA LA KARMELI

"WANAUME WAPO GEREZANI, KABURINI"

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA