100.5 Times Fm yakichangia kituo cha Polisi cha Kawe vifaa mbalimbali

Kituo cha radio cha 100.5 Times Fm, June 21 kilitoa mchango wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kukisaidia kituo cha polisi cha Kawe, wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

 Times Fm imetoa mchango huo baada ya kubaini changamoto mbalimbali za kiutendaji zinazokikabili kituo hicho cha polisi kutokana na upungufu wa vifaa.

Baadhi ya vifaa vilivyokabithiwa kwa kituo hicho cha polisi ni pamoja na viti, meza na vifaa mbalimbali vitavypotumika katika uandishi na uchapaji wa taarifa zao (Stationary).

 Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Camilius Wambura, Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Kawe SSP Mponjoli, aliushukuru uongozi wa kituo hicho kwa hatua walioichukua na kukitaja kama mfano wa kuigwa kwa jamii, vituo vingine pamoja na mashirika mbalimbali katika kutambua kuwa kuisaidia polisi ni kuisaidia jamii.

 Alisema vifaa hivyo vitawasaidia sana katika kurahisha utoaji wa huduma kwa jamii kwa kuwa wamekuwa na changamoto ya upungufu wa vifaa hata kufikia hatua ya kuwaomba wananchi wanaohitaji huduma kujinunulia vifaa kama karatasi za kuandikia taarifa zao. 

“Zamani watu walikuwa wanaona vituo vya polisi kama adui. Lakini hivi sasa ni wakati ambao watu wanatakiwa kuachana na fikra hizo potofu na kuvichukulia vituo vya polisi kama marafiki kwa sababu polisi ni sehemu ya jamii. Jamii inaitegemea polisi na polisi wanaitegemea jamii. Times Fm mmeonesha mfano wa urafiki kwa kusaidia, tunawashukuru sana. Nyie ni mfano wa kuigwa kwa jamii na mashirika mengine.” Alisema Mponjoli. 

Naye mkurugunzi wa Times Fm Radio, Rehure Nyaulawa alitoa wito kwa makampuni na watu mbalimbali kudumisha amani na usalama na kuisaidia polisi kama sehemu ya jamii . 

“Sisi tunaamini kwamba polisi hawako mbali na jamii, shughuli za kipolisi na jamii zinaenda pamoja. Kwa hiyo sisi tutaendelea kuzunguka tukifanya michezo na kuisaidia jamii kadiri tunavyoweza na sio polisi pekee. Hatuwezi kumaliza matatizo lakini tunatoa tunachoweza na tutakuwa kama mfano kwa wengine pia kuweza kujitolea.” Alisema Rehure Nyaulawa. 

Wiki mbili zilizopita Times Fm ilitoa mchango wake kwa chama cha Albino Temeke ili kusaidia kundi hilo kupambana na changamoto za mahitaji zinazowakabiri. 

Michango hiyo hutanguliwa na mechi za kirafiki za mpira wa miguu kati ya timu ya Times Fm (The Dream Team) na timu ya wakaazi wa eneo husika.
Mkurugunzi Mkuu wa Times Fm Radio, Rehure Nyaulawa (kushoto) akikabidhi kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kawe, SSP Mponjoli,sehemu ya mchango wa vifaa mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kukisaidia kituo cha polisi cha Kawe, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pongezi mara baada ya makabidhiano hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI