MISS MANYARA 2014 KUFANYIKA KESHO UKUMBI WA CCM MJINI BABATI

 Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014
Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014 wakiwa wanacheza mmoja ya wimbo watakaoucheza katika siku ya mashindano ikiwa ni moja ya sehemu ya mazoezi. Picha na Woinde Shizza.
Na Woinde Shizza, Manyara 
 Kinyanganyiro cha kugombea Redd's Miss Manyara 2014, kinatarajia kufanyika kesho Jumamosi Juni 14 mwaka huu katika ukumbi wa CCM Mkoa, mjini Babati, ambapo warembo 10 wanatarajia kuchuana. 
 Mkurugenzi wa Mirerani Entertainment, Akon Clement ambaye ni Mratibu wa mashindano hayo alisema mgeni rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mary Nagu. 
 Akon alisema msanii maarufu wa kizazi kipya, Bob Junior kutoka jijini Dar es salaam anatarajiwa kutoa burudani kali wakati akisindikiza michuano hiyo ambapo pia wasanii chipukizi kutoka mjini Babati watashiriki kunogesha. 
 Aliwataja wanyange hao wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kuwa ni Miss Mirerani 2014 Amina Omary, Miss Mirerani namba mbili Catherine Emmanuel na Miss Mirerani namba tatu Happy William. 
Wengine ni Fatuma Salim, Betha Fredrick, Rose Evason, Edna Mushi, Hosiana John, Mary Ruta na Flora Godlizen, ambao ni warembo walioshinda kwenye mashindano ya wilaya za Babati, Hanang' na Mbulu, alisema Clement. 
 Aliwataja wadhamini wa mashindano hayo ni kampuni ya Tanzania Breweries (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd's Original, Open University, Manyara Computer, mireranitanzanite.blogspot.com,libeneke la kaskazini blog na Active Classic Fashion. 
Mratibu huyo alisema kuwa wadhamini wengine wa shindano hilo ni TanzaniteOne, Assey Printing company, Trimus Saloon, Kifaru Agrovet, Winners Hotel, Sarafina Lodge na Kimweri Sport Wear.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

NMB YATOA MSAADA WA SH. MILI. 125 KUBORESHA MIUNDOMBINI KATIKA SHULE 15 ARUSHA