Baada ya
kufikishwa hospital ya wilaya ya kahama kwa matibabu ana baada ya
wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitali kwa huduma .
Nes nisaindieni jaamani nipo pekee yangu ndiyo maneno ya nes naosema na kumuweka katika kiti cha wangonjwa .
Njamaaa muinueni huko tumuweke kwenye kiti kwa ajili ya huduma hospitali ya wilaya ya kahama
jaamani hajakaa vizuri mshikilieni vizuri kwanza
Kijana
mmoja anayekadiriwa kwa na umri wa miaka 30-32 ambaye
hajafahamika majina wala makazi yake ameuawa kwa kupigwa mawe, kisha
kuchomwa moto na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, baada ya kumtuhumu
kutapeli pikipiki.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Nyihogo,
eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri
ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.
Mtuhumiwa
huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo
zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala za
Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.
Aidha
Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya
pikipiki, inadaiwa alimkamata maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga
ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi akiwa amemfunga kamba.
Baada
ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki
huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa
mawe na kisha kumchoma Moto.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugisha Amedhibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetoka jana
majira ya asubuhi saa 5 kijana moja ambaye jina lake alikuweza
kufahamika mara moja alikuwa amekamatwa na mwanachi moja ambapo alikuwa
ametoloka na pikipiki yake maeneo ya nyahanga wilayani kahama .
Aidha
kamanda kamugisha alizidi kuelezea kuwa pamoja na tukio hilo kutokea
kwa kijana huyo jeshi la polisi linawatafuta watu wote walifanya mauji
hayo
MATUKIO KATIKA PICHA:
Comments