RAIS KIKWETE AMFAGILIA MAKALLA KWA UCHAPAKAZI

 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia wananchi katika Kijiji cha Langali Tarafa Mgeta mbele ya Mhe Rais Jakaya Kikwete.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akicheza ngoma ya selo toka Kijiji cha Makuyu.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Kituo cha afya Langali kulia kwake ni mbunge wa jimbo hilo, Amos Makalla.

Na Mwandishi Wetu
 
Rais Jakaya Kikwete amemfagilia mbunge wa mvomero Amos makalla kuwa ni mbunge hodari kwa kutembelea na kuchangia shughuli za maendeleo kata 23 na vijiji 115  yote vya jimbo la mvomero na kati ya  hivyo   vijiji 15 havijawahi kumuona mbunge tangu Uhuru na kufika vijiji hivyo ni kutembea kwa miguu kwa masaa nane kufika katika kila kijiji.

Rais kikwete alifurahishwa na jitihada hizo za mbunge za kufika vijiji vyote kwa muda mfupi na akasema wabunge na madiwani wa ccm wanapaswa kuiga mfano wa makalla wa kuwa karibu na wananchi na kushiriki shughuli za maendeleo Katika kuunga mkono shughuli za maendeleo ukiwemo kuchochea uchumi wa kuinua biashara ya mbogamboga.

 Rais Kikwete amepokea ombi la mbunge la kujenga kwa kiwango cha lami barabara kutoka Mzumbe hadi nyandira ambayo maombi hayo ataelekeza yaingizwe katika bajeti ya serikali mwaka 2015/16.Aidha amewataka wafanyabiashara wa mbogamboga toka tarafa kuboresha ufungaji wa bidhaa zao ili zipate soko zuri ndani na nje ya nchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI