Diwani wa viti maalum Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta) akishiriki kubeba nguzo ya umeme |
Diwani wa viti maalum Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta) kulia akishirikiana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kufukia nguzo za umeme kwenda kata ya Lupingu katika kijiji cha Ntumbati wiki mbili kabla ya kifo chake leo
Gari ya wagonjwa ikiwashusha majeruhi katika Hospitari ya wilaya ya Ludewa waliokuwamo katika ajari
majeruhi wakishushwa hospitari
Wananchi wa kata ya Ludewa wakishuhudia majeruhi waliokuwa wakishushwa katika gari ili kuwatambua
Habari na picha na Matukiodaima.co.tz
DIWANi wa viti maalum kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa Prisca
Kayombo(Zaruta) amekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya katika
ajali ya ajali mbaya ya gari iliyotokea leo asubuhi.
Mashuhuda
wa ajali hiyo waliozungumza na mtandao huu walidai kuwa chanzo
cha ajali hiyo ni gari hilo ambalo walikuwa wakisafiriki kutoka
Lupingu - Ludewa kufeli breki na hivyo kupinduka .
Alisema kuwa wakati akiruka alimsukuma utingo wa basi hilo na hivyo wote wawili utingo na diwani kufunikwa na gari hilo na kupelekea kifo cha diwani huyo huku utingo huyo akiwa mahututi baada ya kubanwa na gari hilo.
"
Diwani huyo amepoteza maisha wakati akiwa njiani kuelekea kujumuika
na wananchi wake katika shughuli ya maendeleo ya kuchimba mashimo ya
nguzo za umeme kuelekea kijijini kwake Lupingu"
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ameeleza kusikitishwa na kifo
cha diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha enzi
wa uhai wakati kwa kushiriki vema na wananchi wa kata yake katika
zoezi la kufyeka na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu.
Alisema
kuwa anakumbuka ni wiki mbili pekee zimepita toka diwani huyo
alipoungana nae katika uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme kwenda
kijiji cha Ntumbati na kuwa hata wakati ajali hiyo
inamkuta bado alikuwa katika harakati za kuwatumikia wananchi wake.
Kwani kati ya madiwani waliokuwa bega kwa bega na wananchi wao na mbunge ni pamoja na diwani huyo ambae alikuwa mstari wa mbele kuona kata ya Lupingu inapata umeme wa uhakika baada ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bila umeme .
Mbunge Filikunjombe alisema atamkumbuka diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo na vile alivyofanya kazi na wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha kifo cha diwani huyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 asubuhi .
Comments