MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA


*Jimbo la Musoma Vijijini:
Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374

*Huduma za Afya Musoma Vijijini 

+Hospital ya Halmashauri/Wilaya: 1
+Vituo vya Afya: 7
+Zahanati zinazotoa huduma:
         28 za Serikali
           2 za Binafsi
+Zahanati mpya zinazojengwa: 11
+Magari ya Wagonjwa (Ambulances): 7

*Kituo cha Afya cha Kata ya Tegeruka:

Kituo hiki cha Afya kinajengwa kijijini Kataryo na kitatumiwa na vijiji vyote vitatu vya Kata ya Tegeruka (Vijiji: Kataryo, Mayani na Tegeruka)

*Ujenzi wa Nyumba ya Daktari:

Mchimbaji Mdogo wa madini,  Ndugu Athanace Makorere Motega, mwenye mgodi wa dhahabu kijijini Kataryo amejenga nyumba ya kisasa kwa ajili ya makazi ya Daktari wa Kituo hicho cha Afya - ahsante sana Ndugu Motega!

*Serikali yatoa Tsh milioni 500:

Serikali yetu imetoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Tegeruka

Wanakijiji kwa kushirikiana na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo, walianza kujenga Zahanati ya kijiji cha Kataryo,  baadae Serikali ikaamua kujenga Kituo cha Afya kwa ajili ya Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu.

Picha Na. 1: 
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akimpa mkono wa shukrani kubwa Ndugu Athanace Mogeka aliyejenga nyumba ya Daktari wa Kituo cha Afya cha Tegeruka 

Picha Na: 2, 3 & 4:
Majengo ya Kituo cha Afya cha Tegeruka, ujenzi unaendelea

SHUKRANI
Wananchi wa Kata ya Tegeruka na Viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuboresha utoaji wa Huduma za Afya Jimboni mwetu - ahsante sana!

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

P. O. Box 6
Musoma

Date: Mon, 16 March 2026







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI