KINANA AUNGURUMA MKURANGA, PWANI NA KUWATAKA VIONGOZI WALIOJILIMBIKIZIA VYEO WAVIACHIE BAADHI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutumia katika mkutano wa hadhara mjini Kimanzichana, wilayani Mkuranga, Pwani , alipoanza zira ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana aliwataka viongozi wa chama na serikali waliojilimbikizia vyeo na kushindwa kutekeleza wajibu wao, waanze kujiuzulu baadhi ya vyeo ili wapatiwe wengine wasio na vyeo kwa lengo la kukiendeleza chama na shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 01.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na chipukizi wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kipala Mpakani, wilayani Mkuranga, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezw
 02.Kinana akikagua gwaride la chipukizi  wakati wa mapokezi hayo.
 Nape (kulia) akiwaongoza wananchi kubeba matofali ya kujengea  jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Adam Malima  (kulia)akiwaongoza wananchi kubeba matofali ya kujengea jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana kuhutubia na kusikiliza kero za za wananchi katika Kijiji cha Kimanzichana.
 Kinana akisalimiana na wananchi
 Mwendesha bodaboda akiwa amelala baada ya kugongwa na gari wilayani Mkuranga katika Barabara Kuu ya kutoka Dar kwenda Mtwara. Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana ulisimama kwa muda katika eneo hilo na viongozi wa CCM akiwemo Kinana waliteremka kwenye magari na kusaidia kubeba majeruhi kuwaweka kwenye magari kuwawahisha kwenda hospitali kwa matibabu.

 Baadhi viongozi na wanachama wa CCM waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinanawakisadia kumbeba mwendesha bodaboda alijeruhiwa baada ya kugongwa na gari wilayani Mkuranga, wakimpeleka kwenye gari ili awahishwe kwenda hospitali kwa matibabu. Baada ya kufika kwenye tukio hilo Kinana alisimamisha msafara wake na kwenda kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.
Gari lilihusika katika ajali na bodaboda likiwa kichakani baada ya kuacha njia
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kimanzichana.
Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA

RATIBA KAMILI YA HARUSI YA DIAMOND, ZUCHU

ZIJUE TABIA 9 ZA WANAWAKE HAWA....

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI 10 ZINAZOONGOZA KWA MAZAO YA KILIMO AFRIKA