TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 MUSOMA LASITISHWA KUFUATIA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA


 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Priomotions ambao ndio waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana kuahirisha onyesho hilo mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.

Kuaihirishwa huko kunafuatia ajali mbaya na ya aina yake iliyopelekea simanzi na majonzi makubwa wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.Waandaji wa tamasha hilo pamoja na Wasanii pia walipeleka vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo,Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu sambamba na Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii Shilole sambamba na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba wakikabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Samsoni Winani.
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani akifafanua jambo kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika kijiji cha SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.Ambapo DK Samsoni alisema kuwa ajali hiyo ni aina yake na haijawahi tokea tangu ajali ya aina hiyo ilivyotokea mnamo mwaka 1996.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akimpa pole Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika katika kijiji cha eneo la SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*