TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI WAREMBO MISS TANZANIA BABATI MKOANI MANYARA

 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini. Na Father Kidevu Blog
 Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.
 Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo
 Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani…
 Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
 wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
 Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
 Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
 Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA

RATIBA KAMILI YA HARUSI YA DIAMOND, ZUCHU

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI 10 ZINAZOONGOZA KWA MAZAO YA KILIMO AFRIKA

ZIJUE TABIA 9 ZA WANAWAKE HAWA....