WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala  wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
 Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.

 Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
 Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
 Baadhi ya Magari ya mizigo yakipakua mahindi na mtama kwenye kituo cha (NFRA) Kanda ya Dodoma.
 Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja naC baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.

Na John Banda

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma kuhakikisha inatafuta suluhisho la haraka la changamoto ya maghala na mifumo ya kuhifadhia mazao inayoikabili taasisi hiyo wakati huu wa msimu wa kununua mazao.

Vilevile Dr. Nchimbi ameelekeza ukarabati wa Maghala ya hifadhi ya “National Milling” yaliyopo eneo la Makole ambayo uwezo wake ni kuhifadhi takribani tani elfu 10 kwa ghala uwekewe mkakati ili kusaidia kuletasuluhisho la haraka la ukosefu wa maeneo ya kuhifadhia mazao yanayoendelea kununuliwa hivi sasa.

Alitoa maelekezo hayo jana alipotembelea kituo cha NFRA Dodoma kukagua maendeleo ya zoezi la ununuzi na uhifadhi wa mahindi na Mtama ambapo alijionea maghala yaliyopo kwa ajili ya kuhifadhia mazao yamejaa na foleni kubwa ya magari yaliyoleta mahindi na mtama kutoka kwa wakulima yakiwa yanasubiri kushusha mazao huku changamoto kubwa ikiwa sehemu ya kuyahifadhi mazao hayo.

Meneja wa NFRA Kanda ya Dodoma Ndg. Mambali alisema kuwa kwa sasa NFRA inanunua mahindi na Mtama kutoka kwa walulima, na kwa mwaka huu, NFRA Kanda ya Dodoma imepanga kununua tani elfu 15 na mpaka sasa tani elfu tatu tu ndio zimeshanunuliwa ambapo tani elfu moja ndio zimefanikiwa kuhifadhiwa kwenye maghala hivyo kunahitajika suluhisho la haraka la sehemu ya kuhifadhi mazao ili zoezi la ununuzi lifanyike kama lilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Dr. Nchimbi amepongeza NFRA kwa kutoa kipaumbele kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei maalumu tofauti na inavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ambapo bei inayonunua kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kilo moja ya mahindi ni shilingi 530 wakati kwa wafanyabiashara wengine inanunua kwa shilingi 500.

Akiwasilisha ombi la vyama vya ushirika vya wakulima kuongezewa kiwango cha tani wanazoruhusiwa kuuza kwa NFRA, Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha Matumaini Kongwa Ndg. Stanley Machakala amemuomba Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwasaidia waongezewe tani zaidi za kuiuzia NFRA kwani huko vijijini bado wakulima wamebakiza mahindi mengi yanayohitajika kuuzwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya ombi hilo, Dr. Nchimbi ameahidi kuwasaidia vyama hivyo vya ushirika vya wakulima kulifikisha suala hilo ngazi husika na kusimamia hadi watakapoongezewa kiwango cha mahindi na mtama
wanachorususiwa kuiuzia NFRA.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE