WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Shirikisho Soka barani Afrika CAF limetoa taarifa kuwa taifa la Kenya π°πͺ limeshindwa kukidhi vigezo vya kuwa mmoja wa mataifa yatakayoandaa mashindano ya CHAN mwakani 2025 mara baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo. Viwanja vyote vilivyopo Kenya havina ubora wa kutumika katika michezo ya FIFA Wala CAF Kwa mujibu wa wakaguzi wa CAF na hata uwanja wa Kasarani unaojengwa pia imeonekana kuwa hautakamilika Kwa wakati. Nafasi hiyo wamepatiwa Rwanda π·πΌ mara baada ya kuonekana wao wamekidhi vigezo vya kuwa wenyeji wa CHAN. CHAN2025 itachezwa katika mataifa matatu ambayo ni Rwanda π·πΌ, Tanzania πΉπΏ pamoja na Uganda πΊπ¬. Uwanja wa Karasani unaoendelea kujengwa.
Baadhi ya wabunge waliokuwa wanasafiri na basi la Shabiby wamepata ajali eneo la Mbande Dodoma, baada ya kugongana na Lori. Akielezea kwa njia simu kuhusu ajali hiyo mmoja wa wabunge waliosafiri na moja kati ya mabasi manne ya Shabiby yaliyokuwa yanawasafisha kwenda kwenye mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki Mombasa Kenya, amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya basi moja kudaiwa kugonga nyuma ya lori lililokuwa limesimama katika Barabara hiyo ya Morogoro - Dodoma. "Aisee, mambo siyo mazuri, basi moja kati ya manne tuliyokuwa tunasafiria limepata ajali na baadhi ya wenzetu wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali za Uhuru na Benjamini Mkapa kwa ajili ya matibabu, hatujui hadi sasa wenzetu wanaendeleaje, nasi bado tupo eneo la ajali," amesema Mbunge huyo. Msafara huo ambao ulitakiwa kupitia Chalinze na Tanga kwenda Mombasa, umejumuisha wabunge na watumishi wa Bunge zaidi ya 120 wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali inayotarajia kuanza kesho Desemba 7...
Ndugu Thomas Omary na mkewe, Bi. Verian Elias, waliopatwa na tukio la kumwagiwa tindikali huko Kasulu, Kigoma, wakipokea faraja kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Bara, John Mongella, walipotembelewa wakiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Profesa Paramagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo na kumteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kurejeshwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali nafasi ambayo aliwahi ishika awali. Awali Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheia na Msigwa alikuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Comments