Dec
19
Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakifanya yao jukwaani.
nakupenda
pia pia aha...Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia
pia ahaa.....Vijana wakiwa kwenye hisia kali jukwaani.
Meneja
wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa
bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village huku akipewa
sapoti na Digna Mbepera.
Digna
Mbepera na Bela Kombo wakimpa back up Aneth Kushaba AK47 kwenye show
zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Majembe ya Skylight Band yakionyesha manjonjo yao jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
Aneth Kushaba na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wao huku Digna Mbepera na Bella Kombo.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka mdogo mdogo.
Birthday girl nae hakubaki nyuma aliunga tela na kuburudika na Skylight Band.
Msanii
wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa
waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.
Kajala akizichomoa tu kwenye pochi lake.
Joniko Flower akisubiria zamu yake.
Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.
Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.
Dec
19
A
PERSONAL JOURNEY: FROM PARASITE IMMUNOLOGY TO DISEASE CONTROL.
MWELECELE
MALECELA
As one who always
thrives on a challenge I set off for my long trip up the Eastern Usambara
Mountains to this place they called Amani. The trip was up a series of
undulating hills until we got to a point where I did not see houses or people.
My fear was supressed by the breathtaking beauty of the drive, the beautiful
forest, and the air getting clearer as we drove up the hill. On arrival at
Amani my fears attacked me again, could I do it how was I expected to live here
almost in the middle of nowhere. I consoled myself by reminding myself that
there were several scientists here and that if they could live here so could I.
My dad had a favourite saying that “its up to you to manage your circumstances”
and that is exactly what I decided to do.
After several weeks of
orientation I was finally designated to work in the helminthology laboratory
where I learnt all about this parasite Wuchereria
Bancrofti, the parasite that spreads bancroftian filariasis. I learnt to
identify microfilariae of Wuchereria
Bancrofti and Onchocerca volvulus.
I learnt to dissect mosquitoes for infective larvae and the lab diagnosis of
several parasites including schistosomes, hookworms, Trichuris etc. At the time
mine was a predominantly wormy world and the people who truly initiated me into
the wonderful world of worms were some great lab technicians and lab assistants
who gave me the best hands on training I ever had. I treasure this training
because it has played a great role in making me who I am today. One lab
assistant liked to remind me that he started working on the month I was born.
It didn’t affect me that they treated me like a kid I just soaked up all the information
that was being given to me and enjoyed every moment. My family sometimes
worried about how i was doing I would phone them from our old handle phones
connected through the tiny exchange to tell them that I was doing fine and that
I actually liked it there.
My early work included
examining the relationship between eosinophilia and helminth parasites, I also
looked at the impact of the trials for vector control for malaria on the
transmission of Bancroftian Filariasis. I also worked with the late Prof Chris
Curtis to control culicines in Muheza town using polystyrene beads.
I then went on to do my
Msc and PhD at the London School of Hygiene and Tropical Medicine of the
University of London, where I worked on filarial infection in cats. The cats
was an experimental animal model that provided a lot of current knowledge in
the understanding of the pathogenesis of filarial infection. The work I did
focused on understanding how parasites evaded the hosts immune system and my
findings indicated that there were surface immunoglobulins of the host that
actually protected the parasite. This added to the body of knowledge on
asymptomatic microfilaraemics people who have microfilariae but have no overt
symptoms of the disease.
Dec
18
rime Minister of the
Australian Government, Honourable Tony Abbott
--
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION
President
of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho
Kikwete has sent a condolence message to the Prime Minister of the
Australian Government, Honourable Tony Abbott (MP) following the Sydney
café siege which occurred on the 16th December, 2014 and claimed the lives of two people.
The message reads as follows:
“The Honourable,
Tony Abbott (MP)
Prime Minister of Australia,
Canberra, AUSTRALIA.
Honourable Prime Minister,
I am deeply saddened by the Sydney cafe siege on the 16th
December 2014 that claimed the lives of 2 people. The attack was indeed
received with great shock in my country particularly at this time when
the world is seen to be working together to end the scourge.
As
the people of Australia continue to grieve for the loss of their loved
ones, the Government and the people of the United Republic of Tanzania
reiterates its continued support to the Australian Government on the
fight against terrorism and wish the bereft families a full and fast
recovery from the tumor.
Please accept, Honourable Prime Minister the assurances of my highest consideration”.
Issued by:
THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM
18TH DECEMBER, 2014
Dec
18
UNITED REPBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION
The
Southern African Development Community (SADC) Secretariat has organized
the SADC students essay writing competition for the year 2015. The
essay writing competition is intended to broaden knowledge of the
secondary school going population on SADC activities. The competition is
open to all students from Form 1 to Form 6. The students are required
to begin researching on the topic prior writing and submitting the same
to their Heads of School.
The 34th SADC Summit of Heads of State and Government deliberated and agreed that the topic for the year 2015 be: "Leveraging
the Region's Diverse Resources for Sustainable Economic and Social
Development through Beneficiation and Value Addition". Discuss how this
would result in Sustainable Economic Development.
The
following set of questions below are meant to guide students when
responding to the question above. Thus, on answering the question,
students should answer all the questions listed below as follows:
Dec
18
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka akizungumza na
Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano kwenye
hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Sehemu
ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka.
Sehemu ya Umati wa Waandishi wa Habari.Picha na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii
Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick
Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake
kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika
kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti
ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini
Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya
kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa
moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Dec
18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.
Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994
UZOEFU WA KAZI:-
Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.
Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.
Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014
Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.
Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994
UZOEFU WA KAZI:-
Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.
Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.
Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014
Dec
18
1. Ismail Seif, mkazi wa Kigamboni.
Kwa nini hutembelei baadhi ya maeneo hasa
nje ya Tandika, Temeke na Buza naomba ututembelee usisubiri hadi
uchaguzi ufike kwani huku maeneo ya Kurasini kuna kero nyingi tunahitaji
kukuona siyo hadi wakati wa kampeni.
Jibu: Nashukuru sana Seif, kwa bahati mbaya maeneo
ya Tandika, Temeke na Buza na Kurasini yapo jimbo la Temeke ambalo liko
chini ya Abbas Zuberi Mtemvu. Nitamjulisha ili aje kuwatembelea.
Dec
18
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Taifa, Kharist Michael Luanda akitoa
taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini
kote kitaifa leo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Dodoma.Picha na Sifa Lubasi -HabariLeo
---
MAGAZETI kiushabiki kabisa yaliandika mtikisiko, yakaandika CCM
yagalagazwa kila kona, lakini kwa taarifa hii ya ushindi wa asilimia
80.58 inadhihirisha kushindwa kwa ajenda ya magazeti kutengeneza njia ya
kuing’oa CCM madarakani.
Aidha kwa takwimu hizo inaonesha ndoa ya ukawa inahitaji maboresho zaidi ili ngome za vyama zisiliwe na kuacha msambaratiko.
Lakini la msingi ipo haja ya wananchi kufahamu siasa, uwongo na ukweli, na pia kuangalia kama wanatazama kazi za watu au fikira wanazopandikizwa.
Dec
18
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Willy Kitima kuwa Msaidizi wa Rais –
Nyaraka(Documentation) kuanzia Alhamisi iliyopita, Desemba 11, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kitima alikuwa Mratibu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Biashara nchini ya Business Action Against Corruption (BAAC)Tanzania.
Taasisi hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Madola na Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB)na Taasisi ya Uendelezaji Sekta Binafsi nchini ya PPSF.
Bwana Kitima pia amewahi kuwa Mkrugenzi Mtendaji wa Shirika la Kufutilia Nyendo za Rushwa Kimataifa la Transparency International (TI) nchini. Aidha, ana ujuzi wa shughuli za benki na vyombo vya habari.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Desemba, 2014
Dec
18
Balozi wa Tanzania nchini Austria ambaye ana makazi mjini
Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo akipokea heshima kutoka Gwaride
rasmi kwa ajili ya Balozi huyo ambalo katika hafla ambayo iliendeshwa
katika viwanja vya Hofburg.
Balozi wa Tanzania nchini Austria ambaye ana makazi mjini
Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo; mapema mwezi huu alikabidhi Hati
za Utambulisho (Letter of Credence) kwa Mhe. Dkt. Heinz Fischer, Rais
wa Austria. Shughuli hizi zilifanyika katika ukumbi maarufu wa Maria
Teresa uliopo katika kasri ya wafalme wa zamani wa “Austro-Hungarian
Empire” mjini Vienna. Gwaride rasmi kwa ajili ya Balozi mpya iliendeshwa
katika viwanja vya Hofburg.
Dec
18
Madhari
ya gati la Bandari ya Bukoba
Sehemu
ya kupumzikia abiria ya Bandari ya Bukoba.
Wajumbe
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye ngazi za kupandia
kwenye meli zinazotia nanga kwenye Bandari ya Bukoba.
Timu ya
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili
kwenye Bandari ya Bukoba, walipofika kujionea bandari hiyo kongwe iliyopo
kwenye fukwe za Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Waliotangulia mbele ni Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wengine ni baadhi ya wajumbe wa
msafara huo kutoka kushoto ni Bw. Omary Abdallah, Bibi Zena Hussein (Wapili
kushoto) na Bw. Julius Edward (Kulia).
Dec
18
Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro.
Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete.
Wafungwa wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama
inavyoonekana katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na
trekta wakiwa gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu
mbalimbali za Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa
nchini. Kwa wastani Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku
Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Mkuu wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa
Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014
kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi
huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Milioni
2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya
Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments