RAIS AKATAA MTU YEYOTE KUTUMIA JINA LAKE


 
Mwaka mmoja kabla ya kiongozi wa taifa la North Korea Kim Jong Un kuchukua mamlaka agizo lilitolewa kwa mtu yeyote aliye na jina kama lake kulibadilisha ili kuendeleza utamaduni wa utawala wa familia ya Kim.
Kulingana na nakala za kimataifa zilizopatikana na Runinga ya KBS nchini Korea Kusini zilizo na maagizo ya utawala wa Kim Jong wa Pili vitengo vya polisi na jeshi vilitakiwa kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa.
Agizo hilo lilitolewa mnamo mwezi January mwaka 2011 mda mfupi baada ya Kim Jong Un kuteuliwa kama mrithi wa babaake.
Kim Jong wa Pili alifariki mwezi Disemba mwaka huohuo.
''Vitengo vyote vya chama na mamlaka ya usalama ni sharti viweke orodha ya watu walio na majina ya Kim Jong Un na kuwafundisha vile watakavyobadilisha majina yao'',ilisema nakala hiyo ambayo baadhi yake ilitangazwa moja kwa moja na runinga ya KBS.
Mpango huo ulishirikisha kubadilisha majina katika stakhabadhi rasmi,ikiwemo katika kadi za usalama wa jamii na vyeti vya masomo.

Maafisa pia waliagizwa kukataa vyeti vya kuzaliwa vya watoto wachanga walio na majina ya Kim Jong Un.

Vilevile Mamlaka ziliagizwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayelalamika ama kueneza uvumi.
Chimbuko la agizo hilo rasmi halikuweza kuthibitishwa huku wizara ya Seoul ikikataa kuthibitisha iwapo madai hayo ni ya ukweli.

Lakini Afisa mmoja wa utawala wa Pyong yang alidai kwamba Utawala huo uliwapiga marufuku raia wake kutumia jina la rais wa kwanza wa taifa hilo Kim wa pili Sung na mwanawe Kim jong wa Pili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA