MJASIRIAMALI WA VYAKULA VYA MIFUGO AJISHINDIA PIKIPIKI YA STARTIMES




Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopo Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.


Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5,  Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo ya  tatu ya kujishindia pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.  
Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akionyesha nyaraka za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akichezesha droo ya bahati nasibu kumpata mshindi wa nne. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi nyaraka za pikipiki mshindi wa droo ya tatu ya kujishindia pikipiki ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

Namba ya smartkadi ya king’amuzi cha mshindi wa nne wa droo ya pikipiki ya mwezi Aprili inayoendeshwa na StarTimes ikionekana katika luninga mara baada ya kuchezeshwa kwa droo ya bahati nasibu mbele ya waandishi wa habari. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.


 Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif akipiga simu kumjulisha mshindi ushindi wake.
Na Dotto Mwaibale
 MKAZI wa Kijitonyama Dar es Salaam, Mary Luis Tumsifu (40) ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza vyakula vya mifugo na ufugaji amekabidhiwa zawadi ya pikipiki baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya mwezi ya bahati nasibu inayoendeshwa na StarTimes Tanzania.

Akizungumza wakati anakabidhiwa pikipiki yake Tumsifu amebainisha kuwa amefurahia sana zawadi hiyo kwani hakutegemea kama angeweza kushinda kwani alilipia kutazama vipindi anavyovipendelea.

“Sikutarajia kama nitajishindia pikipiki lakini tayari ndiyo bahati imekwishaniangukia mimi. Ni kweli nilikuwa nafahamu kuhusu bahati nasibu hii kupitia njia mbalimbali kama vile kutumiwa ujumbe mfupi pamoja na matangazo. 

Kwa kawaida huwa nalipia kifurushi kile kikubwa cha shilingi 30,000/- cha Kili. Mimi ni mpenzi sana wa ‘Series’ na mwanangu anapenda kuangalia chaneli ya watoto ya ‘Nickelodeon’. Hivyo huwa sina budi kulipia ili mimi na mwanangu tufarahie vipindi tunavyovipenda.” Alisema  Tumsifu

“Mimi ni mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo lakini pia ni mfugaji. Kusema kweli hii zawadi imekuja kipindi ambacho sijaitarajia hivyo nashindwa hata kuelezea nitaitumia kwa namna gani. Naweza kuifanya kama biashara au mimi mwenyewe nikajifunza na kuwa dereva bodaboda.”  Alisema kwa masihara huku akicheka.

Akizungumzia kuhusiana na imani waliyonayo wateja juu ya bahati nasibu hii kuwa ni uzushi, Tumsifu alifafanua kuwa, “Kwanza kabisa ningependa kuwatoa hofu na kuwahakikishia wateja na watanzania kuwa kitu kama hicho hakipo. 

Kwa mfano mimi sifahamiani na mtu yeyote StarTimes, huwa nalipia vifurushi vya mwezi kama wateja wengine lakini nimebahatika nimeshinda. Hivyo basi nawaomba wengine pia waondoe mawazo hayo na kushiriki pindi wanapoambiwa wafanye hivyo.”

“Nashukuru sana kwa zawadi hii, ninaahidi nitaitumia vema ili inisaidie katika shughuli zangu. Wito wangu, kwanza kabisa kwa StarTimes, nawapongeza kwa huduma bora wanazotupatia wateja wao tena kwa bei nafuu, ninawaomba wazidi kuboresha zaidi, wasikilize maoni yetu ili tuzidi kufurahia.” Alihitimisha. Tumsifu

Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif aliwataka wateja wa kampuni hiyo kuchangamkia hii fursa kwa kujiunga zaidi na vifurushi ili waweze kuburudika na pia kushinda.

“Ningependa kutoa wito kwa wateja wetu kujiunga zaidi kwani zawadi bado zipo na pongezi kwa waliojishindia. Zawadi hizi tunazozitoa ni sehemu ya mpango wa StarTimes kurudisha fadhila kwa wateja wake kuwa waaminifu na kutuunga mkono tangu awali tulipoanza kufanya kazi. 

Tunafahamu kuwa hiki tunachokitoa hakitoshi hata chembe lakini tunachoweza kuwaahidi ni kuwapatia huduma bora na nafuu kwa asilimia mia moja.” Alihitimisha Hanif

Mbali na kukabidhiwa kwa mshindi huyo, StarTimes pia walichezesha droo kumtafuta mshindi wa nne wa pikipiki ambapo Bw. Samson Mollel, mkazi wa Arusha ambaye amenunua king’amuzi cha kulipia cha NYOTA kinachouzwa kwa shilingi 34,000 siku moja kabla ametajwa kuwa ni mshindi. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA