Dk Mwele Malecela ajitosa urais CCM




MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu Dk Mwele Malecela mtoto wa Makamu wa zamani wa CCM John Malecela ni miongoni mwa wana CCM ambao wamejitosa kugombea urais kupitia CCM.
Dk Mwele kesho amepangiwa na CCM kuchukua fomu za kuomba kugombea urais. Ratiba ya CCM iliyotolewa jana Makao Makuu ya chama hicho mjini hapa inaonesha kuwa licha ya Dk Mwele, mwingine ambaye atachukua fomu hiyo kesho ni Nicholaus Mtenda ambaye pia amejitokeza kuomba kugombea urais kupitia CCM.
Dk Mwele katika maisha yake mengi kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa mtumishi katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambako alianza kazi akiwa kijana na akapanda hadi kuwa mtafiti mkuu na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.
Licha ya kukulia katika familia ya mwanasiasa maarufu nchini, lakini Dk Mwele hajawahi kujitokeza hadharani kushiriki kwenye masuala ya siasa. Kama akichukua fomu hiyo kesho, atakuwa ni mwanamke wa pili kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Mwanamke mwingine ni Balozi Amina Salum Ali wa Zanzibar. Jana Waziri wa Malisili na Utalii, Lazaro Nyalandu na wanachama wengine wawili wa CCM walichukua fomu za kuwania urais. Nyalandu alikuwa wa kwanza kufika katika ofisi za CCM kuchukua fomu akiwa amefuatana na familia yake na wafuasi wake kadhaa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA