Sehemu
ya Wakazi wa mji wa Bukoba Mkoani Kagera wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege
wa Bukoba, wakimsubiri kumlaki Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, tayari kwa kupokea fomu ya
wanaCCM wa kumdhamini.
Wadau wa CCM wakijadiliana jambo.
Ndege iliyombeba Mh. Edward Lowassa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM
Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze wakati alipowasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN
MICHUZI.
Mh. Lowassa katika tabasamu.
Umati
wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa
umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye
ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, leo Juni 15, 2015.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Katibu wa UWT wilaya ya Bukoba
Vijijini, Agness Bashemu alipokuwa akitoa taarifa fupi ya namna ya
kumkabidhi fomu hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini,
Yussuf Ngaiza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoba, Dkt. Aman Kaborou akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC) Bukoba, Nazir Karamagi akuzungumza machache mbele ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze akizungumza mbele ya umati wa wanaCCM
pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, na
kutangaza kwamba yeye pia ni mmoja ya wana Safari ya Matumaini.
Shangwe kila kona.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara
baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate
ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye
Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye
majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi
Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, Wakati akitoa shukrani zake kwa kumdhamini ili
apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania,
kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya
wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wanaCCM
pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015,
mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili
apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania,
kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Comments