BONGO MOVIES WAKABIDHIWA KADI ZA UANACHAMA WA SIMBA

1Wasanii wa sanaa za maigizo maarufu kama ‘Bongo Movies’ wanaoishabikia klabu ya Simba leo wamekabidhiwa kadi za uanachama wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha siku ya Simba ijulikanayo kama ‘Simba Day’ ambayo huadhimishwa kila ifikapo Agosti 8 kila mwaka.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva ndiye aliyewakabidhi kadi hizo wasanii wakiongozwa na Jacob Steven ‘JB’, Mtitu, Monalisa pamoja na Odama ambao wote kwa pamoja wakekuwa wanachama wapya wa klabu hiyo kuanzia sasa.

2Baada ya kukabidhiwa kadi zao JB alizungumza kwa niaba ya wenzake akisema anajisikia fahari kubwa kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Simba kwasabu klabu hiyo ni moja kati ya timu kubwa barani Afrika  yenye historia ya aina yake katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla na anafurahi kuwa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo.
“Simba ni klabu kubwa iliyojaa historia ya aina yake na mimi najivunia kuwa mwanachama wa klabu hii japo timu yetu imekuwa haifanyi vizuri sana kwa siku za hivi karibuni”, amesema JB.
3“Klabu ya Simba imeanza kutambua mchango wa wasanii kwenye timu yao na ndio imekuwa klabu ya kwanza nchini kukabidhi kadi kwa wasanii hadharani kama hivi, lakini usishangae kuona vilabu vingine vimeiga na kufanya hiki ambacho kimefanywa leo na klabu ya Simba”, aliongeza.
Katika hatua nyingine, Simba imesema imeialika timu ya FC Leopards kuja kucheza mchezo wa kirafiki katika kusherehekea siku ya Simba Day itakayoadhimishwa Agosti 8 mwaka huu. Rais wa Simba Bw. Aveva ameongeza kuwa, siku hiyo kutakuwa na mechi ya utangulizi kati ya viongozi wa Simba watakao kipiga dhidi ya wasanii wa Bongo Movies kabla ya mtanange wa Simba SC dhidi ya FC Leopard.
5

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA