DK KAWAMBWA AJIKITA KUCHANGIA KWENYE UJENZI WA MADARASA NA MITAJI BAGAMOYO MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa akizungumza na wanachama wa vikundi vya ujasiriamali vya jipe moyo na kiroho safi,vilivyopo Mwavi kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
 MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo,

DIWANI wa kata ya Fukayose,Ally Ally Issa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkenge katika kata hiyo,wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo,dk Shukuru Kawambwa aliyoianza jimboni hapo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali jimboni humo ambapo amechangia zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji.
Aidha ametoa zaidi ya sh.mil.10 kuchangia vikundi viwili vya ujasiriamali kwenye kila kata kwa ajili ya kukopeshana ambapo kati ya vikundi hivyo vimewezeshwa sh.mil.1 hadi mil.1.5.
Hayo aliyasema ,kijiji cha Mwavi,Mkenge na Fukayose wakati wa ziara yake inayolenga kupeleka mrejesho kwa wananchi kuhusiana na hatua anazozichukua kufuatilia kero zao zinazowakabili.
Dk.Kawambwa alisema jimbo hilo lina jumla ya kata 11 na kila kata ameichangia kati ya mifuko 100-150 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa .
Alieleza kuwa amehakikisha mfuko wake wa jimbo unaunga mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo na kuwezesha wajasiriamali.
Mbunge huyo alisema,ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona bado shule nyingi zinapambana na changamoto ya uhaba wa madarasa na vikundi kukosa mitaji.
Hata hivyo,dk.Kawambwa aliahidi kutoa matofali 1,000 katika kitongoji cha Kalimeni na kwa kijiji cha Kitopeni ameshawapa ardhi yenye heka 6 na fedha kwa ajili ya kujenga shule na tayari wameanza .
“Nimeona suala la madawati limemalizika vizuri kwa ushirikiano wa wadau,halmashauri na ofisi ya wilaya ya Bagamoyo,tumevuka kwa hili lakini tatizo ni majengo “
“Nitaelekeza nguvu zangu katika ujenzi huu kulingana na uwezo uliopo pamoja na kusupport akina mama na vijana kwenye vikundi vyao”alisema dk.Kawambwa.
Aliiomba jamii washirikiane kwa pamoja kwenye ujenzi wa madarasa ili kufanikisha lengo lao la kuondokana na upungufu wa madarasa.
Akizungumzia jambo la ujasiriamali aliwaomba wananchi wajishughulishe na kutumia fursa zilizopo ikiwemo mikopo kutoka kwa mbunge,halmashauri ili kujiendesha kimaisha.
Nae diwani wa kata ya Fukayose,ambae pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo,Ally Ally Issa,alivitaka vikundi vya ujasiriamali kurejesha mikopo kwa wakati.
Alisema kwasasa vikundi ambavyo havina uaminifu havitofumbiwa macho na vitachukuliwa hatua za kisheria.
Ally alisema mitaji haitoshi lakini halmashauri hiyo imeshawezesha vikundi mbalimbali kuanzia sh.mil.2 hadi mil.4 kulingana na vigezo vilivyopo na namna kikundi kinavyorejesha .
Alieleza kata hiyo ina tatizo kubwa la maji,migogoro ya wakulima na wafugaji,miundombinu ya barabara kuwa korofi ikiwemo barabara ya kuelekea Mkenge na zahanati ya kijiji cha Fukayose kukosa gari la wagonjwa /maabara na upungufu wa nyumba za walimu .
Dk Kawambwa anaendelea na ziara yake jimboni hapa akiwa kata ya Makurunge na January 12 atakuwa  kata ya Magomeni.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI