RAIS MAGUFULI AMUWAJIBISHA PROF. MUHONGO KWA SKENDO YA MCHANGA WA MADINI




RAIS John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo (pichani), ajipime,ajitathmini na hatimaye aachie ngazi haraka kwa kutokuwa makini kusimamia mchanga wa adini uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi, hivyo kulikosesha taifa fedha nyingi.

Pia Rais Magufuli ameivunja Bodi ya TMAA pamoja na kumfukuza kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa TMAA hiyo pamoja na kuwasimamisha kazi watendaji wa bodi hiyo kuanzia leo.

Ameamrisha vyombo vya dola kuwafanyia uchunguzi watendaji wote hao waliokuwa wanahusika na kutathmini thamani ya mchanga wa madini uliokuwa unasafirishwa nje. Ameagiza wote wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

Pia ameagiza aliyekuwa Kamishna wa Madini, aliyekuwpo wizarani hapo miaka minne iliyopita, akamatwa na kuchunguzwa na hatimaye kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Rais Magufuli, ametoa maagizo hayo baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi ya mchanga huo kutoka kwa Tume aliyoiunda Machi mwaka huu.

Tume hiyo imebaini katika makontena ya mchanga 277 yliyopo bandarini yana madini ya aina mbalimbali yanayofikia thamani ya sh. trilioni 1.4. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA