Hivi Ndivyo Wauaji Kibiti Walivyochoma Gari, Pikipiki


Gari na pikipiki vilivyokuwa vikitumiwa na askari wa usalama barabarani vikiwa vimechomwa moto na kuteketea.
Licha ya kuwaua askari wawili wa kikosi cha usalama barabarani jana wakiwa kazini karika eneo lililo kati ya Bungu na Jaribu wilayani Kibiti jana, wauaji hao pia walichoma moto gari na pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na wana usalama hao.
Waandishi wetu waliofika eneo la tukio leo hii mchana, walishuhudia mabaki ya vyombo hivyo vya usafiri ambavyo habari zinasema gari hilo lilikua aina ya Escudo na pikipiki aina ya Kawasaki.
Muonekano wa karibu wa gari hilo baada ya kuchomwa.
“Hawa askari walikuwa watatu, mmoja mwanamke alifanikiwa kukimbia wakati wenzake wakiuawa, wakati anakimbia, alitupa kofia na kuvua shati akibaki na blauzi tu ili asionekane na kufuatwa na wauaji,” alisema mtu mmoja aliyekutwa eneo la tukio, aliyekataa kutajwa jina lake kwa kuhofia usalama wake.
Wakati huohuo, wakati wanakijiji wakijiandaa tayari kwa mkutano ambao ulidaiwa kuandaliwa na kutakiwa kuhutubiwa na mkubwa wa mojawapo ya vikosi vya ulinzi, mkutano huo uliahirishwa ghafla, kwa maelezo kuwa kuna dharura.
“Watu walikuwa wanajiandaa kuja kusikiliza mkubwa gani anaongea, lakini majira ya saa kumi tukatumiwa ujumbe kuwa mkutano hautakuwepo, tutapewa taarifa zaidi baadaye,” alisema mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa, ambaye naye alikataa kutajwa jina wala kupigwa picha, akisema wao ni walengwa wakubwa wa mauaji hayo.
Pikipiki iliyochomwa moto ikionekana kwa karibu.
Jana mchana, askari wawili wa kikosi cha usalama barabarani waliuawa wakiwa kazini na watu ambao hawakujulikana, lakini kukiwa na hisia kuwa ni walewale ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiendesha mauaji ya viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, CCM na askari pasipo kujulikana hasa nini lengo lao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA