4x4

Mazishi ya Ally Yanga, Shinyanga


Ali Yanga enzi za uhai wake
SHINYANGA: Aliyekuwa shabiki maarufu wa Yanga, Ally Mohammed ‘Ally Yanga’ amezikwa leo nyumbani kwao mkoani Shinyanga baada ya jana kuagwa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kusafirishwa kupelekwa kwao kuzikwa.
Mwili wa marehemu Ali Yanga ukipelekwa makaburi kwa maziko
Ally maarufu kama Ally Yanga alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma, juzi Jumanne.
 
Shabiki huyo alikuwa maarufu kwa kujipaka masizi na kuweka kitambi cha bandia pale alipokuwa uwanjani akiishangilia Yanga na wakati mwingine timu za taifa.
Ally ambaye pia alikuwa kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwili wake ulipokelewa na wanachama wa chama hicho kama picha zinavyoonyesha.

Simanzi na Vilio Vyatawala Kuagwa kwa Shabiki wa Yanga, Ally Yanga

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana
Post a Comment