FAHAMU DALILI KUU ZA AWALI ZA MIMBA KUSHIKAKukosa siku zako sio dalili pekee ya kushika mimba, bali kuna dalili zingine utakazoziona. Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza kukufanya ukose siku zako, hivyo soma dalili za mimba ili ikusaidie kupata uhakika.

Moja, ni mabadiliko katika siku zako. Hii kitaalamu tunaita spotting. Unaweza kushika mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo ambazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango na siku za damu hubadilika.

Pili, ni kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa. Hii inasababishwa na ongezeko la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

Tatu, ni kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapotoka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni ya ‘projestroni’ ambayo husababisha kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa chakula au koromeo.

Nne, ni uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa na sababu. Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko la homoni ya ‘projestroni’ na mama utajikuta unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

Kwa elimu zaidi kuhusu dalili hizi kuu za awali kabisa zinazoashiria mimba imeshika soma hapa>https://www.checkpregnancy.com/implantation-signs/

Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia ujumbe huu,

Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE na kui SAVE page hii ili usipitwe na habari mpya za kila siku, kwa maoni, ushauri au jambo lolote usisite kunicheki admin wa Online News Tz 0769421630 whatsapp au simu ya kawaida kupitia 0656 581877 au email :emanuelmsoka77@yahoo.com
 — with Haika BarakaEsther Philemon Lishnhu and Emanuel Kichawele.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI