ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kulia), akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Spice leo  makutano ya Mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Dar es Salaam leo.Taasisi hizo zitashirikiana katika nyanja za teknolojia na Kilimo kwa lengo la kuunganisha nguvu za umoja ili kuwapunguzia wananchi umasikini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Seleman Msuya

ZAIDI ya wanachama 500 wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wanatarajiwa kushiriki mafunzo maalum ya kufungua msimu wa kilimo cha Papai salama.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkikita, Adam Ngamange wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Ngamange alisema mafunzo hayo yatafanyika Februari 24 mwaka huu yatabeba ujumbe 'Papai salama open speech' kwa lengo la kuunganisha walaji, wazalishaji na wataalam wa kilimo hicho.

Alisema baada ya tafiti kufanyika wamegundua mkanganyiko mkubwa wa taarifa hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi mabadiliko katika kilimo cha Papai yatatokea.

"Tafiti zinaonesha watalaam wanatofautiana kwenye idadi ya miche, uchimbaji wa mashimo, umwagiliaji maji na utiaji mbolea hivyo mafunzo haya yataweka washiriki kwenye mstari ili kukidhi ubora na ulinganifu wa soko la ndani na nje," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yatawakutanisha wabobezi na watendaji mbalimbali katika kilimo hicho kipya cha Papai salama yatakuwa  na awamu tatu tofauti ili kujenga misingi imara katika kuleta unafuu wa uzalishaji papai.

Alisema Mkikita imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wakulima wa Tanzania hasa wanaolima papai, mchaichai, mhogo na pilipili kichaa.

Aidha, Ngamange alisema pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kupokea ugeni kutoka nchini Uturuki kutambua fursa za zao la papai nchini.

Pia alisema wanachama wa Mkikita wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo Nchini Israel kuanzia Machi 11 mwaka huu na kugharimu dola za Marekani 2,000.

Halikadhalika Mkikita imesaini makubaliano ya ushirikiano  na Taasisi ya Hope For All ambayo ina wanachama zaidi ya 5,000 ili waweze kushirikiana kwenye nyanja za teknolojia na kilimo.

Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Hope For All Edgar Mwamfupe alisema matarajio yao ni kuona mkulima anaheshima katika jamii.

Mwamfupe alisema kupitia Mkikita wanachama wao watafikia kwenye umilionea kwa kuwa kuna fursa za soko na biashara.



 Ngamange akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya semina ya mafunzo ya Kilimo biashara cha Papai Salama.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari  na kuelezea ni kwa nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi masikini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari  na kuelezea ni kwa nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi masikini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui na Adam Ngamange.
 Mratibu wa Ziara ya Utalii Kilimo Israel, Bw. Kizito (kulia), akielezea umhimu wa ziara hiyo  pamoja na faidha watakazozipata watakaokwenda.
 Mfanyabishara Adamjee (kulia) akielezea kuhusu kilimo cha pilipili kichaa na faida zake. Adamjee amekubali kujiunga na Mkikita ili kusaidiana kutafuta masoko ya zao hilo ndani na nje ya nchi.
 Ngamange akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akielezea kazi mbalimbali za mtandao huo
 Askofu Mwamfupe na Adam Ngamange wakitliana saini makubaliano ya ushirikiano

 Mtaalamu wa Kilimo cha Zao la Pilipili Kichaa, akielezea faida ya zao hilo  pamoja na matumizi mbalimbali ya pilipili
 Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema akielezea taratibu za wanachama na wasio wanachama  jinsi ya kushiriki kwenye semina ya Kilimo cha Kisasa cha Papai Salama.
Mmiliki wa Spice Hotel Ltd, Mwangaba (kulia) akizungumza na uongozi a Mkikita uliokutana naye baada ya kufanya mkutano na wanahabari kwenye hoteli hiyo ya Kisasa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA