Serikali
imejipanga kuwajengea Kisima cha kisasa watu wenye mahitaji maalum
kitachoweza kuhudumia Kaya 26 zenye jumla ya watu 56 wenye ukoma na
wazee katika Kambi ya Samaria Hombolo jijini Dodoma.
Hatua
hiyo inakuja mara baada ya wakazi wa kambi ya Samaria kueleza
changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo; ukosefu wa maji salama,
changamoto za matibabu kwa kukosa bima za afya, uchakavu wa magodo kwa
ajili ya malazi, uhaba wa chakula cha uhakika.
Changamoto
hizo zimeibuliwa wakati ya Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa
alipoambatana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso Mei
23, 2018 katika Makazi ya watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wazee na
watu wenye ukoma.
“Watu
wenye mahitaji maalum ikiwemo wenye ukoma wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto ya maji eneo la Samaria, sisi kama Serikali tumedhamiria
kuwajengea kisima cha kisasa kitakachotoa maji baridi na kuweza
kuhudumia makambi haya pamoja na kijiji chote cha Samaria”.alisema Naibu
Waziri Ikupa
Naye
Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameiagiza timu
ya waataalamu kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kuanza kazi
hiyo mara moja.
“ Naagiza timu ya wataalamu kuja kupima maeneo ambayo yatafaa kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho” .alisema Aweso
Kwa
upande wake, Katibu Chama cha Wenye ulemavu Samaria, Richard
Kongawadodo aliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua ya kujenga kisima
cha maji baridi kitakachosaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali
na kusaidia katika shughuli za maendeleo ikiwemo za kilimo, umwagiliaji
na matumizi mengineyo.
“Naipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutujali watu wenye mahitaji maalum hasa
sisi wenye ukoma kwani tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya kukosa
maji ya uhakika na salama, hivyo ujenzi wa kisima hicho utaleta tija
hususan katika shughuli za kilimo ili kujipatia fedha na kukidhi
mahitaji muhimu”,alisisitiza Kongawadodo
Kwa
kumalizia Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Mheshimiwa Mathayo Ndahilo
aliwataka wanakijiji wa Samaria kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali
pindi inapohitajika ili kufanikisha adhma ya ujenzi wa kisima hicho.
AWALI:
Kituo
cha Samari kilianza mwaka 1993 ambacho kipo umbali wa Kilometa Moja na
nusu kutoka Hombolo mjini mkoani Dodoma, kwa sasa kinahudumia jumla ya
watu wenye ukoma 52 wanaotoka katika Kaya 26 Kijijini hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa
akizungumza jambo na wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria lilipo
Kata ya Hombolo Bwawani mkoni Dodoma alipowatemnbelea kutatua changamoto
wanazokabiliana nazo tarehe 23 Mei, 2018, kulia kwake ni Naibu Waziri
Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso.
Naibu
Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso akiwahakikishia
wakazi wa Samaria utatuzi wa changamoto ya maji inayowakabili kwa
kuahidi kuanza uchimbaji wa kisima cha maji baridi baada ya kufanya
ziara alipoambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye
Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa Mei 23, 2018.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa
akiwasiliza baadhi ya wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria
alipowatembelea Mei 23, 2018 kwa kutatua changamoto ya maji kwa kuahidi
kuanza ujenzi wa Kisima cha maji baridi Kijijini hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa na
Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji (katikati) pamoja na Meneja
Kanda ya Kaji kutoka Wakala wa Uchimbaji wa Visima na mabwawa, Khalifu
Utali wakiwasililiza wakazi wa Makazi ya wenye ukoma walipowatembelea
Mei 23, 2018.
Diwani
wa Kata ya Hombolo Bwawani, Mathayo Ndahilo akitoa maelezo mafupi
kuhusu Kituo cha Watu wenye mahitaji maalum cha Samaria wakati wa Ziara
ya Manaibu waziri Mhe Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Wenye Ulemavu) na Jumaa Aweso (Wizara ya Maji na
Umwagiliaji) walipotembelea Makazi hayo Mei 23, 2018.
Baadhi
ya watu wenye ukoma wanaoishi katika makazi ya Samaria wakimsikiliza
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa
(hayupo pichani) wakati alipowatembelea kutatua baadhi ya changamoto
wanazokabiliana nazo kambini hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa
pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso
wakikabidhi msaada wa chakula kwa Katibu wa Chama cha Katibu Chama cha
Wenye ulemavu Samaria, Richard Kongawadodo kwa ajili ya wanaoishi na
ukoma kilichopo Hombolo Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa
pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso
wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Kambi la Samaria Mzee Simion Lucas
walipotembelea kwenye kambi hiyo Mei 23, 2018.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)
Comments