MABINTI TGGA TEMEKE WAPINGA NGONO,MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

 Girl Guides wa Wilaya ya Temeke, wakikataa ndoa na mimba za utotoni  wakati wa maadhimisho a Siku ya Mtoto wa Kike yaliyoandaliwa na uongozi wa  TGGA Temeke, kwenye Ukumbi wa Idd Nyundo Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Katikati aliyevaa miwani ni Mgeni rasmi Mwalimu Hawa Chanafi wa Shule ya Tandika. Chanafi alimwakilisha Meya wa Temeke.

TGGA Temeke hadi sasa ina wanachama 5200. Tamasha hilo lilihudhuriwa na wanafunzi kutoka shule za Wailes, Likwati, Keko Magurumbasi, Tandika, Chamazi na Uwanja wa Ndege.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
 Kamishna wa Tanzania Girl Guides Association -Temeke, Komba (kushoto) , akiwa na Mgeni rasmi, Hawa Chanafi pamoja na Mwenyekiti wa TGGA Temeke, Mary Gabusa wakipiga makofi wakati wa maadhimisho hayo.
 Girl Guides wakiwa na bango lenye ujumbe wa Nguvu ya Mtoto wa Kike
 Wakiimba wimbo wa Taifa

 Kamishna wa TGGA Temeke, Komba akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ya Mtoto wa Kike ya Kupinga ndoa na mimba za utotoni.Komba aliwataka mabinti ili kutimiza malengo yao muda wote wajilinde dhidi ya watu wabaya wanaotaka kuwaharibia maisha yao
 Girl Guides wakifurahi

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamazi, wakitumbuiza kwa wimbo wa Taarabu
 Mabinti kutoka Shule ya Msingi Chamazi Dar es Salaam, wakitumbuiza kwa ngoma yenye maudhui ya kukataa ngono, mimba na ndoa za utotoni
 Wanafunzi wakiigiza kwa kumkamata na kumpeleka Polisi mwanafunzi aliyeigiza kama baba ambaye alikuwa analazimisha kumuozesha kwa mzee  mtoto wake ambaye ni mwanafunzi
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakiigiza kusikitika jinsi baadhi ya wanaume wanavyotoa vishawishi kwa watoto wa kike kwa lengo la kufanya nao ngono na kuwapatia mimba.
 Girl Guides kutoka Shule ya Msingi Wailes wakifanya shoo ya mitindo ya mavazi
 Mgeni rasmi, Chanafi akihutubia katika maddhimisho hayo ambapo aliwaasa watoto wa kike kukataa ngono,mimba na ndoa za utotoni ili watimize ndoto zao za maishao yao ya baadaye.
 Chanafi akisisitiza jambo kwa kuwaambia watoto wa kike wasikubali kulaghaiwa na mtu yeyote kufnya nao ngono za utotoni  ili wasonge mbele kimaisha
 Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho kumalizika
Mgeni rasmi akiagana na Girl Guides

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA