HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA WAWAJIBIKE, WAKOME TABIA YA KUSUBIRI URITHI MALI ZA WAZAZI

 Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe  akipata chakula cha mchana  wanafunzi  wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Na Richard Mwaikenda-Dar 
WANAFUNZI waliomaliza Kidato cha Nne,  wametakiwa kuachana na tabia ya kupoteza muda  kusubiri kurithi mali za wazazi wao, bali wajitambue  kwa kufanya kazi kwa bidii  kujiletea maendeleo.

 Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe  wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.

“Kila mmoja ajitambue kivyake,, simama wewe kama wewe, jitambue wewe ni nani, ukijiami kama unaweza na utaweza kweli. Mkome kutegemea kurithi mali za baba zenu,” aliwaaasa Mwamfupe.

“Msiruhusu ndoto zenu zife, hata kama  mtakumbana na mazingira magumu majumbani kwenu, mzishikile msiruhusu ndoto zenu zife, Kawaida wewe ndiyo unaamua kuwa tajiri au masikini , utajiri uko kichwani kwako,” alisisitiza Mwamfupe huku akipigiwa makofi na wanafunzi.

 Mwamfupe, hakusita kujitolea mfano yeye kuhusu maisha yake ya ujana, ambapo aliwaeleza kuwa licha ya utajiri wa babake, lakini yeye aliamua kujitegemea tangu akiwa anasoma na kwamba alipokuwa ana miaka 19 alinunua gari aina ya Toyota Corola (Mayai).

 Pia, kupitia kipaji chake cha kucheza mpira na ngoma za asili kilifanya kwa mara ya kwanza apande ndege  kwenda Romania kuiiwakilisha Taifa katika Tamasha la Ngoma. 

Pia aliwahi miliki bendi ya Muziki wa dansi.Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger aliwataka vijana wenzie  wanapoingia mitaani  ambako kuna mambo mengi mazuri na mabaya , inatakiwa wajiwekee mipango  yao ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu.

“Mungu alituumba watu wote tukiwa na bongo moja, hakuna mwenye bongo mbili, hivyo  hata wewe unaweza,  ondoa hofu utashinda. Fanyeni mambo yenu mazuri mapema ili baadaye mkizeeka mje muishi vizuri.”

Naye Mkuu wa Kitengo cha Wanawake na Watoto wa Taasisi hiyo, Juliana Mushi aliwaasa watoto wa kike kuacha tabia ya kujihusisha na umalaya ili waje kuwa wazazi wazuri wa baadaye.  Aliwataka badala ya kujihusisha na mambo hayo mabaya bali wawe wanajishughulisha na  mambo ya uzalishaji mali, ikiwemo ujasiriamali.

Wakati wa mafunzo hayo wanafunzi walipata wasaa wa kila mmoja kuelezea kuwa ndoto yake ya maisha atakuwa nani. Baadhi wanataka kuwa wajasiriamali, madaktari, mawaziri, walimu, wakandarasi, wasanii maarufu, waandishi wa habari  na mmoja aitwaye  Davis Eugene yeye alitaka awe Rais wa Nchi.


Taasisi hiyo ina mpango wa kuanzisha Klabu za mafunzo kama hayo katika shule mbalimbali nchini na kwa Dar es Salaam wameanza kuweka klabu katika shule hiyo ya Makongo Juu. Lengo ni kuwataka wanafunzi waliomaliza elimu hiyo kuwa na kazi ya kufanya wanaposubiri matokeo ya kujiunga kidato cha tano na wanaoshindwa kujiunga waendeleze ndoto zao.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe  (Kulia), akimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akijieleza jinsi atakavyokabiliana na maisha baada ya kumaliza shule..
 Wanafunzi wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo
 Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger akiwa tia moyo wanafunzi hao
 aitwaye  Davis Eugene ambaye ndoto yake ni kuwa Rais wa Nchi.
 Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Meneja Utawala wa Taasisi hiyo, Fides Uisso alipokuwa akiwaeleza jinsi ya kuwa na uthubutu wa kutimiza ndoto zao
 Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Vijana, Harrison  alipokuwa akifundisha jinsi ya kujiandaa kimaisha kwa kuanzisha miradi mbalmbali ya maendeleo.
 Fides Uisso akibadilishana mawazo na wanafunzi kwenye viwanja vya shule hiyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI