MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

 Wanachama wa Namaingo wakishangilia wakati wa sherehe za kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2019 leo katika Makao Makuu yao, Ukonga, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
 MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mollel AKIZUNGUMZA WAKATI WA SHEREHE HIYO AMBAPO ameitakia mafanikio mema Taasisi ya Namaingo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka 2019.



Na Richard Mwaikenda, Ukonga.

MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mollel ameitakia mafanikio mema Taasisi ya Namaingo katika 
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka 2019.

Akizungumza wakati wa sherehe za kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2019 iliyoandaliwa leo Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Ukonga, Dar es Salaam,

 Mbunge Mollel, alisema ni faraja kubwa Namaingo kuongozwa na Biubwa Ibrahim ambaye ni mwanamke jasiri, shupavu na mwenye maono ya kuwaendeleza Watanzania.

Alisema kuwa Mkurugenzi Biubwa anahitajika sana ili kuongeza nguvu kusaidia kuleta maendeleo nchini na kuipeleka nchi katika uchumi wa kati kwani amewahamasisha wanachama wake katika mikoa 19 kujikita katika kilimo na ufugaji, hivyo kuwa mingoni mwa watu wa kwanza kuandaa malighafi zitakayotumia katika viwanda.

Aliwaasa vijana kuacha kubweteka kwa kusubiri kila jambo wafanyiwe na wazazi wao, bali washiriki katika uzalishaji na kujitengenezea utajiri kupitia kwenye ujasirimali kwa kutumia ardhi na rasilimali na mikopo yenye riba nafuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa. Kila Halmashauri katika mapato yao inatakiwa kutenga asilimia 10 kwa ajili ya kuwakopesha vijana , wanawake na walemavu kuendeleza miradi.

"Tuutafakari mwaka 2019, tukijua kabisa mali ipo shambani na utajiri utaupata kwa kutumia mikono yako mwenyewe. tusibweteke bali tuupige vita umasikini, kwani umasikini ni dhambi," alisema Mollel.

Namaingo imeazimia mwaka 2019 kujikita katika utekelezaji wa miradi ya kilimo, ufugaji wa samaki, nyuki, hivyo kuwasaidia wanachama wao kujiongezea kipato.

Katika hafla hiyo, viongozi wa dini walimpongeza Biubwa kwa mafanikio aliyowapatia wanachama wa Namaingo kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kumtakia heri ya kuishi miaka mingi duniani.

"Binadamu unatakiwa ufanye jambo moja kubwa ili uishi maisha marefu duniani. Mungu hajawahi umba mtu masikini,haitakiwi mtu afe bila kufanya jambo lolote kubwa duniani.Biubwa ni mfano wake tayari amefanya jambo kubwa tunamtakia heri ya kuishi maisha marefu, nakutabiria utaishi hadi miaka 120.". Alisema Mchungaji Michael Mwakibinga wa Kanisa la Rise and Shine la Mwamposa alipokaribishwa kutoa neno.

Naye Sheikh Maulid Kidege,alimpongeza Biubwa kwa kuwa na uwezo wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanachama wake kiasi cha wengine kufanikiwa kimaisha na kwamba kwa kitendo hicho anapata baraka hivyo kutakiwa kuwa miongoni mwa watu wanaotakiwa kuishi miaka mingi.

Alisisitiza kwamba ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote , kwanza inatakiwa uwe na elimu zifuate mali au utajiri na kinachofuata ni kuwa mfalme. 

sherehe hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya wanachama wa Dar es Salaam, wawakilishi kutoka mikoa 19 nchini, viongozi wa siasa na wa dini pamoja na watoto yatima. walijumuika pamoja kula vyakula na vinywaji/



 Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahimu akihutubia wakatika wa sherehe hiyo, ambapo aliwataka wanacnhi kuukemea umasikini  hata kwa kuuzomea hadi uondoke 
 Baadhi ya wanachama wakiwa katika shere hizo


 Maulid na Shabaan Wakiomba dua wakati wa sherehe
 Mwanachama Sad Ngamilo akitoa taarifa ya miradi iliyofanikiwa katika mikoa ya Iringa na Njombe
 Mwakilishi wa Mikoa ya Kusini, Abdalah Said akitoa taarifa za mafanikio ya miradi ya Namaingo k
 Katibu wa Namaingo, Janeth Bungu akisoma risala ya wanachama wa Namaingo
 Mollel akisisitiza jambo wakati wa sherehe hiyo
 Biubwa akihutubia
 Sasas ni wakati wa msosi

 Watoto Yatima wakipata mlo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA