CHONGOLO APOKELEWA KWA VILIO KILOLO


 KATIBU Mkuu, Daniel Chongolo ametoa siku 10 kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kufika Kijiji cha Uhambingeto, Jimbo la Kilolo ambako mradi wa maji umekwama.


Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi hao kuangua kilio mbele ya Chongolo wakati Diwani wa Kata ya Uhambingeto, Tulinumtwa Mlangwa alipokuwa anatoa taarifa ya kukwama mradi huo.


Mradi wa Maji Uhambingeto unatekelezwa na Mkandarasi Mshamind Co LTD, kwa gharama ya Sh2.1 Bilioni huku 1.3 Bilioni akikabidhiwa.


Chongolo amesema haiwezekani fedha itolewe na mradi huo ushindwe kukamilika wakati wananchi wanahitaji maji.


"Waziri wa Maji afike Uhambingeto ndani ya siku kumo, aje atoe pole kwa wananchi kwa kuchelewa kwa mradi huu lakini pia atengeneze utaratibu wa wananchi wapate maji.


Alisema anataka inapofika Septemba 30, wananchi wa Uhambingeto wawe wamepata maji.

"Sijaridhishwa na huu mradi, hatuwezi kwenda namna hii, hapa tatizo nimkandarasi twende tukakae tuchukue hatua. Cha msingi hapani maji," amesema Chongoloo.


Alisema kwa haraka ili wananchi hao wapate maji anatoa matenki mawili makubwa wakati, ujenzi wa tenki ikiendelea.


Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga amesema ameshahangaika kufuatilia mradi huo bila majibu.


"Bei ya maji ya kunywa huwa inafika Sh5000 kwa ndoo, Serikali ilitenga bajeti lakini Mkandarasi ndio tatizo kubwa," alisema Chongolo.


Awali Diwani wa Kata hiyo ya Uhambingeto Tulinumtwa Mlangwa alishindwa kujizuwia na kuangua kilio mbele ya Katibu Mkuu CCM  Dainiel Chongolo kufuatia kutokamilika kwa  Wakati mradi wa Maji  na kupelekea wananchi kuendelea kutumia maji ya bwawa ambayo siyo safi na salama.


Mlanga  alisema kuwa mkandarasi amekuwa mwiba mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo na kupelekea chuki kwa chama na Serikali kutokana na ucheleweshwaji wa mradi huo.


"Ndugu katibu mkuu kuna miradi ya maji ambayo iliukuta mradi huu  unatekelezwa na imeshakamilika,tunahitaji ng1uvu ya ziada ili kuokoa Afya ya wananchi"Alisisitiza Mlanga"


Alisema Mkandarasi alifika kijijini hapo kujitambulisha akiahidi mpaka Februari, utakuwa umekamilika.


"Lakini alirudi mwezi wa nne akasema watakamilisha mradi huo, wananchi wa Uhambingeto wanachotaka ni maji, wasipopata maji tutarudije 2025?" amesema.



Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA