YALIYOJIRI ZIARA YA DKT NCHIMBI; ASISITIZA SUALA LA MBOLEA, MSHIKAMANO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Nchimbiakihutubia wananchi katika ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa, amesisitiza serikali  kusambaza  mbolea kwa wakati na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima lakini pia amewaomba watanzania kudumisha upendo na mshikamano kwa mstakabali wa utulimu na usalama wa nchi.


Katika ziara hiyo ya siku 10 katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya , Njombe na  kuhitimishwa mkoani Ruvuma Aprili 23, 2024 yenye lengo la kukihuisha chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kutoa elimu juu ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama.


Dkt Nchimbi ambaye kwa upande wangu mimi ambaye nilikuwa miongoni mwa wanahabari waliokuwa kwenye msafara wake  nilimuona ni mtu mwenye msimamo, mkweli na uhakika.


 Katika ziara hiyo yenye mafanikio aliambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM,  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MSIMAMIZI MKUU 
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA

DKT NCHIMBI AAGIZA UJENZI UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA UKAMILIKE HARAKA