EWURA YAHAMASISHA WADAU KUPELEKA HUDUMA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA VIJIJINI KAHAMA

 MENEJA EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi. Walter Christopher, amewahamasisha wamiliki wa vituo vya mafuta kupeleka huduma ya nishati safi ya kupikia vijijini ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau wa mafuta Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga .

Mhandisi Christopher amesema kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kulinda afya, kuokoa gharama na muda sambamba na kulinda Mazingira.

“Nishati Safi ya kupikia ina manufaa makubwa kwetu binadamu na mazingira kwa ujumla hivyo nawaomba wamiliki wa vituo vya mafuta muunge mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za  kupeleka huduma hiyo  kwa wananchi wa vijijini ili waweze kutumia nishati safi ya kupikia.”amesema Mhandisi Christopher

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPSOA Wilaya ya Kahama, Bw. Alley Abeid Salum ameishukuru EWURA kwa elimu na anaamini kuwa itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wadau wa mafuta.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA