Ukiwa ni mfanyakazi, sehemu ya tatu Wafanyakazi wengi wakipata kazi wanakuwa na tabia ya kuoa wake za watu au wanawake waliokuwa kwenye mahusiano na wanaume wengine. Katika kipindi hicho, utakuta wanaume walioporwa wake wao bado wako katika harakati za kujitafuta kimaisha au bado wanasoma. Kwa sababu ya wafanyakazi hao kuwa na ajira nzuri, hunyakua wake za watu, kuwaoa, na kuwahamishia mikoa mingine. Baada ya hapo huwazalisha watoto, wakidhani kwamba kumzalisha mwanamke ndiyo kumemaliza na kumfanya ampende. Lakini kiukweli, mahusiano hayo huwa yamejengwa juu ya msingi wa ajira na fedha—na hali hiyo hutokea kwa sababu yule aliyenyang’anywa mpenzi hana ajira wala uwezo wa kifedha. Hata hivyo, kadri siku zinavyosonga mbele, wanawake huanza kurudisha mapenzi kwa wanaume wao wa zamani, hasa baada ya wanaume hao kuanza kuwa na maisha mazuri wakiwa na ajira au fedha nyingi, pengine hata zaidi ya wale waliowanyang’anya wake. Mwisho wa siku, mke uliyemuoa kwa kumwanyang’anya lazima atarudi kwa ...
Comments