Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025, kesho Septemba 17, 2025 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia kwa kishindo Tanzania Visiwani baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu kampeni zake Tanzania Bara katika mikoa tisa ya Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora na Kigoma.
Kesho Jumatano anatarajia kufanya mikutano mikubwa Mjini Magharibu, Kusini Unguja na Kaskazini Unguja. Alhamisi Septemba 18 ataendelea na kampeni Kaskazini Unguja Wilaya ya Kaskazini A na Ijumaa Septemba 19, 2025 atafanya mambo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Comments