Katibu Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kikongosi ametumia mikutano ya kampeni za Chama hicho kuwaaambia vijana wasiandamane na badala yake waandamane katika kutafuta fedha.
Maneno hayo ya hekima na busara ameyarudia tena katika mkutano wa kampeni wa CCM katika Jimbo la Kalenga Iringa, Septemba 6, 2025 kwa kuwaasa vijana kutothubutu kuingia kwenye mtego huo.
"Kumekuwa na tabia ya watu kuwahamasisha vijana kwenda kufanya vurugu lakini waende kwenye maandamano yasiyorasmi ya uvunjifu wa amani.Andamaneni kutafuta fedha, andamaneni kulima, andamaneni kufanya biashara.
“Andamaneni kufanyabiashara ambazo zitawaingizia kupato ninyi pamoja na familia zenu.Msiende kuandamana kwa masilahi ya watu binafsi ambao familia zao hazipo ndani ya taifa letu, wao wanako kwa kukimbilia wewe huna pa kukimbilia.” Amesisitiza Kihongosi.
Comments