Huyu jamaa alipata dola milioni 660 kupitia YouTube. Lakini hatengenezi video.
Anaitwa Scooter Braun. Hivi ndivyo alivyofanikisha hilo.
1/ Mwanzo
Rudi mwaka 2002. Scooter ametoka tu kuacha chuo. Na anajaribu kuingia kwenye sekta ya muziki.
Tatizo moja. Hana mtandao wowote. Na anatakiwa ajitafutie nafasi ya kuingia.
Kwa hiyo anaanzisha sherehe. Matamasha, vichekesho vya usiku, na maonyesho ya mitindo. Muda mfupi baadaye, hizi zinakuwa sherehe kubwa zaidi mjini. Na wakubwa wa muziki wanaanza kumtazama.
Scooter anapata kazi kwenye lebo ya muziki. Anajifunza undani na mbinu za sekta hii haraka sana.
Na yuko karibu kutumia ujuzi huo vizuri sana.
2/ Kujitegemea
Sogeza mbele hadi 2007. Jamaa anaacha kazi na anatafuta dola 1,800 za kuanzisha kampuni yake ya usimamizi wa vipaji.
Sasa anachohitaji ni kipaji.
Ndio anapoona kijana akifanya muziki kwenye YouTube. Jina lake ni Justin Bieber.
Scooter anamfuatilia mama yake Bieber, anawapangia ndege kwenda Atlanta, na anamsainisha Justin mkataba wa muziki.
Kisha anafanya jambo la ajabu. Anatumia mitandao ya kijamii kwa kiwango cha juu kabisa. Anaandaa maonyesho kokote atakapoweza. Kisha anayachapisha yote kwenye mtandao wa YouTube.
Leo inaonekana kawaida. Lakini mwaka 2007 haikuwa hivyo.
Ndani ya miaka 3 tu, Bieber anajaza kumbi kubwa za show duniani kote.
Scooter ameshaanza safari yake. Lakini bado hatujaanza kabisa.
3/ Kujenga biashara
Scooter anaendelea kusaini wasanii. Ariana Grande, Demi Lovato, J Balvin. Kila mmoja wao anashika nafasi za juu kwenye chati.
Kwa nyuma ya pazia, anafikiria zaidi ya muziki tu. Anashughulikia ziara, vipindi vya TV, filamu, matangazo ya biashara, mitandao ya kijamii, udhamini, na uwekezaji.
Anambadilisha kila msanii kuwa mashine ya kutengeneza pesa.
Anapata mamilioni kupitia asilimia ndogo tu ya kila dili.
Wakati wa kuwekeza hizo pesa.
4/ Kupanda ngazi
Sasa SB anaenda kununua mali.
Ananunua hisa kwenye kampuni ya usimamizi wa muziki ya Drake Management
Ananunua lebo kubwa ya muziki wa country
Anawekeza mapema kwenye Uber, Dropbox, na Spotify
Scooter anapanua wigo. Anajenga hazina kubwa ya mali.
Vipande vyote vya mchezo vimeshakamilika. Kimebaki kitu kimoja tu.
5/ Kufunga Dili Kubwa
Aprili 2021. Simu ya Scooter iliita.
Mwanzilishi wa HYBE anampigia. Mojawapo ya kampuni kubwa zaidi za muziki duniani.
HYBE wanaitaka biashara ya Scooter. Yote.
Wanapatana juu ya bei. Dola bilioni 1.1.
Scooter anamiliki 60%. Thamani yake: dola milioni 660.
Sio vibaya kwa uwekezaji wa dola 1,800.
Mytake: Usidharau udogo wa mtaji wako. Pesa kidogo, uelewa wako, bidii na bahati vinaweza kukufanikisha sana hata mara 1000.

Comments