WASIRA:TANZANIA HAINA NCHI ADUI ILA YAPO MATAIFA YANAUMIZWA NA KASI YA MAENDELEO YETU.



 

*Awasihi Vijana  kutokubali kucheza ngoma ya wanaoogopa kasi ya nchi kujiondoa kundi la ombaomba*


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM amewataka vijana kutokubali kutumika kuvuruga amani na utulivu nchini nchini madai ya kudai haki kwa kuwa kufanya hivyo kuna athari kubwa kwa na taifa kwa ujumla.


Amesema, ingawa Tanzania haina nchi adui, lakini yapo baadhi ya mataifa yanayoumizwa na kasi ya maendeleo ya taifa wakiamini nchi inaelekea kujikomboa kiuchumi hivyo kuondoka katika kundi la kuomba misaada kutoka kwao.


Wasira ameeleza hayo leo Desemba 1, 2025 alipokuwa akizungumza na Wahitimu 1249 wa kozi mbalimbali katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Karume- Zanzibar.  


"Tanzania haina nchi adui yaani rasmi kusema sisi nchi yetu adui yetu yule pale, Tanzania hatuna, lakini sio kweli kwamba duniani watu wote wanatupenda, hiyo nayo siyo sahihi.


"Wako wengine wakiona tunafanya maendeleo makubwa wananuna, wapo, wengine wana sababu zao si sababu zetu, wasingependa tujitegemee kwa kuwa tukijitegemea tutaachana na habari ya kwenda kwao kuomba, kwa hiyo wangependa wakati wote iwe 'spoon feed' yaani tunakaa tunangoja msaada msaada msaada.


"Wakiona chama kinafanya jitihada ambazo zitatuondoa katika kuombaomba, hawapendi. Wakiona Zanzibar imepiga hatua miaka 60 na miaka mitano tu iliyopita hapa ya awamu ya nane wanashtuka, wanashangaa hawapendi," alisema. 


Akisisitiza wasira alisema "yapo baadhi ya mataifa yakiona Tanzania inajenga reli tunaunganisha nchi za Afrika Mashariki na kati, tunaimarisha TAZARA, tunaunganisha Burundi na Congo DR, wakisikia kwamba tunataka kuunganisha Tanga na Musoma kwa ajili ya biashara na Uganda na wakisikia kwamba tunataka kujenga reli kutoka Mtwara kwenda Mbambabay kwa ajili ya biashara ya Malawi na 'Mozambiki' (Msumbiji) wanajua kwa kufanya hivyo Tanzania itakuwa kitovu cha maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki. Hatuna ugomvi na nchi yoyote lakini wako watu hawapendi kuona tunajitegemea."


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...