WAANDISHI TUACHE UNAFIKI, GAMONDI AMEITENDEA HAKI TAIFA STARS

Ifike wakati na sisi waandishi tupunguze au tuache kabisa Unafki kwenye mpira wakati mwingine sisi tunaanzisha mijadala ambayo ni dhaifu kabisa.

Huyu Gamondi kachukua timu kwenye nyakati ambazo hakupata game time ya kutosha kuweza kuitegeneza timu lakini amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuijenga timu imara ambayo kila mtu ameona ilivyocheza.

Kwenye Afcon zote tulizoshiriki hii ndo Afcon ambayo tumefunga kila mechi na wachezaji wameonyesha ubora mkubwa, ukiwauliza wachezaji wanakuambia Gamondi amewabadilisha kuanzia mentality yao na kujiona wanaweza kufanya kitu.

Inakuaje mwandishi hutaki kuona mchango wa Gamondi kuanzia performance ya timu ya matokeo? Yaani unataka kuaminisha watu kuwa Gamondi hakuna alichobadilisha??.

Bila kumlinganisha na makocha waliopita nadhani apewe sapoti kwa alichokifanya na anastahili pongezi, na kama huoni impact ya Gamondi kwenye timu ya Taifa then hustahili hata kuongelea mpira watu wakakusikiliza.

Our future is bright, waliopita walifanya makubwa ila Gamondi amefanya zaidi na anatakiwa kupongeza, tuache kusukuma agenda ambazo hazijengi ili tu kuonekana unatoa maoni tofauti. 

I was here @ashrafjr_21



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

Wasifu wa Kizza Besigye

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA